Yohana MT. 7
7
1NA baada ya haya Yesu akawa akitembea katika Galilaya: maana hakutaka kutembea katika Yahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua. 2Na siku kuu ya Wayahudi, siku kuu ya vibanda, ilikuwa karibu. 3Bassi ndugu lake wakamwambia, Ondoka bapa uende Yahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. 4Kwa maana hakuna mtu afanyae neno kwa siri, na yeye mwenyewe anataka kujulikana. Ukifanya haya, jidhihirishe kwa ulimwengu. 5Maana hatta ndugu zake hawakumwamini. 6Bassi Yesu akawaambia, Haujafika wakati wangu; wakati wenu sikuzote u tayari. 7Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi: bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. 8Pandeni ninyi kwenda kushika siku kuu hii; mimi sipandi bado kwenda kushika siku kuu hii: kwa kuwa wakati wangu haujatimia bado. 9Alipokwisha kuwaambia haya, akakaa katika Galilaya.
10Hatta ndugu zake walipokwisha kupanda, ndipo yeye nae akapanda kwenda kuishika siku kuu, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri. 11Bassi Wayahudi wakamtafuta katika siku kuu wakanena, Yuko wapi huyo? 12Kukawa manungʼuniko mengi katika makutano kwa khabari zake; wengine wakisema, Yu mtu mwema; na wengine wakisema, Sivyo, bali anawadanganya makutano. 13Illakini hapana mtu aliyemtaja kwa wazi kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi. 14Hatta ilipokuwa katikati ya siku kuu Yesu akapanda, akaingia hekalui akafundisha. 15Wayahudi wakastaajabu, wakinena, Amepataje huyo kujua elimu, nae hajasoma? 16Bassi Yesu akawajibu akasema, Elimu yangu siyo yangu, illa yake yeye aliyenipeleka. 17Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua khabari ya elimu hii kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. 18Yeye anenae kwa nafsi yake tu, hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anaetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyu ni wa kweli wala ndani yake hamna udhalimu. 19Aliyewapeni torati si Musa? wala hapana mmoja wenu aitendae torati. Mbona mnatafuta kuniua? 20Makutano wakajibu, wakasema, Una pepo; ni nani anaetafuta kukuua? 21Yesu akajibu, akawaambia, Nalitenda kazi moja, nanyi nyote mnastaajabu. 22Kwa sababu hii Musa aliwapa tohara, si kwamba yatoka kwa Musa bali kwa babu zenu: nanyi siku ya sabato humtahiri mtu. 23Bassi ikiwa mtu apashwa tohara siku ya sabato, torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato? 24Msihukumu hukumu ya macho, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.
25Bassi baadhi ya watu wa Yerusalemi wakanena, Huyu si yeye wanaemtafuta illi kumwua? 26Na kumbe! ananena waziwazi wala hawamwambii neno? Yumkini wakuhwa wanajua kwa hakika ya kuwa huyu ni Kristo! 27Lakini huyu twamjua atokako, bali Masihi atakapokuja, hakuna ajuae atokako. 28Bassi Yesu akapaaza sauti yake hekaluni, akifundisha, akisema, Mimi mnanijua, na nitokako mnakujua; wala sikuja kwa naisi yangu, illa yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. 29Lakini mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, nae ndiye aliyenituma. 30Bassi wakatafuta kumkamata: lakini hapana aliyenyosha mkono wake illi kumshika kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado. 31Watu wengi katika makutano wakamwamini: wakasema, Atakapokuja Kristo, je! atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu? 32Mafarisayo wakawasikia makutano wakinungʼunika hivi kwa khabari zake: bassi Mafarisayo na makuhani wakuu wakatuma watumishi illi wamkamate. 33Bassi Yesu akanena, Bado muda kitambo nipo pamoja nanyi, kiisha nakwenda zangu kwake yeye aliyenipeleka. 34Mtanitafuta, wala hamtaniona; nami nilipo, ninyi hamwezi kuja. 35Bassi Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, Huyu atakwenda wapi hatta sisi tusimwone? Atakwenda kwa Utawauyiko wa Wayunani na kuwafundisha Wayunani? 36Neno gani hilo alilolisema, Mtanitafuta wala hamtaniona; na nilipo mimi, ninyi hamwezi kuja? 37Hatta siku ya mwisho, siku ile kubwa ya siku kuu, Yesu akasimama, akapaaza sauti yake, akinena, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. 38Aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyonena, mito ya maji ya uzima itamtoka tumhoni. 39Neno hili alilisema katika khabari ya Roho, ambae wale wamwaminio watampokea khalafu: kwa maana Roho Mtakatifu alikuwa bado kuwapo, kwa sababu Yesu alikuwa bado kutukuzwa.
40Bassi watu wengi katika makutano waliposikia neno lile, walinena, Huyu hakika yake ndiye nabii yule. 41Wengine walinena, Je! Kristo atoka Galilaya? 42Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daud, na kutoka Bethlehemu, kijiji kile alichokaa Daud? 43Bassi yakaingia matangukano kwa ajili yake. 44Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hapana mtu aliyenyosha mkono wake illi kumshika.
45Bassi wale watumishi wakawaendea makuhani wakuu na Mafarisayo, nao wakawaambia, Mbona hamkumleta? 46Wale watumishi wakajibu, Hajanena kamwe mwana Adamu aliye yote kama huyu anavyonena. 47Bassi Mafarisayo wakawajibu, Je! ninyi nanyi mmedanganyika? 48Ni nani katika wakubwa amwammiye, au katika Mafarisayo? 49Lakini makutano hayo wasioifahamu torati wamelaaniwa. 50Akawaambia Nikodemo (ni yule aliyemwendea usiku, maana ni mmojawapo wao), 51Je! sharia yetu humhukumti mtu kabla ya kumsikia kwanza na kujua atendavyo? 52Wakajibu, wakamwambia, Wewe nawe umetoka Galilaya? Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii. 53Wakaenda killa mtu nyumbani kwake:
موجودہ انتخاب:
Yohana MT. 7: SWZZB1921
سرخی
شئیر
کاپی
کیا آپ جاہتے ہیں کہ آپ کی سرکیاں آپ کی devices پر محفوظ ہوں؟ Sign up or sign in
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.