Yohana MT. 5
5
1BAADA ya haya palikuwa na siku kuu ya Wayahudi; Yesu akapanda kwenda Yerusalemi.
2Na huko Yerusalemi penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiehrania Bethesda, nayo ina matao matano. 3Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, na waliopooza, wakingoja maji yachemke. 4Kwa maana kuna wakati malaika hushuka akaiingia ile birika, akayatibua maji: bassi yeye aliyeingia kwanza baada ya maji kutibuliwa, akaponea ugonjwa wote uliokuwa umempata. 5Na huko palikuwa na mtu, amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane. 6Yesu alipomwona huyu amelala, akijua ya kuwa amekuwa hali hii siku nyingi, akamwambia, Wataka kuwa nizima? 7Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; bali wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. 8Yesu akamwambia, Simama, jitwike kitanda chako, ukaende. 9Marra yule mtu akawa mzima, akajitwika kitanda chake, akaenda. Bassi ilikuwa sabato siku ile. 10Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, si halali kwako kujitwika kitanda chako. 11Akawajibu, Yeye aliyenifanya kuwa mzima, ndiye aliyeniambia, Jitwike kitanda chako, ukaende. 12Bassi wakamwuliza, Yule mtu aliyekuambia, Jitwike kitanda chako ukaende, ni nani? 13Lakini yule aliyeponywa, hakujua ni nani; maana Yesu amejitenga, kwa sababu palikuwa na watu wengi mahali pale. 14Baada ya haya Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima: usitencle dhambi tena, jambo lililo baya zaidi lisije likakupata. 15Yule mtu akaenda zake, akawapasha Wayahudi khabari ya kwamba Yesu ndiye aliyemfanya kuwa mzima. 16Kwa sababu hiyo Wayahudi wakaanza kumwudhi Yesu, wakitaka kumwua, kwa kuwa alitenda haya siku ya sabato. 17Yesu akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hatta sasa, nami ninatenda kazi. 18Bassi kwa sababu hii Wayahudi wakazidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na haya alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu.
19Bassi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Mwana hawezi kutenda neno kwa nafsi yake, illa lile amwonalo Baba analitenda; kwa maana yote atendayo yeye, hayo na Mwana ayatenda vilevile. 20Maana Baba ampenda Mwana, amwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; na kazi kubwa zaidi kuliko hizi atamwonyesha illi ninyi mpate kustaajabu. 21Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha awatakao. 22Maana Baba hamhukumu mtu aliye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; 23illi wote wamheshimu Mwana kama wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyempeleka. 24Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima. 25Amin, amin, nawaambieni, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hayi. 26Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake; 27akampa mamlaka ya kufanya hukumu kwa sababu yu Mwana wa Adamu. 28Msistaajabie haya: kwa maana saa inakuja, ambayo watu wote waliomo makaburini watakapoisikia sauti yake, nao watatoka: 29wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliofanya manyonge kwa ufufuo wa hukumu.
30Mimi siwezi kufanya neno kwa nafsi yangu: kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo, na hukumu yangu ina haki: kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mwenyewe, bali mapenzi yake Baba aliyenipeleka. 31Mimi nikijishuhudia nafsi yangu, ushuhuda wangu si kweli. 32Yuko mwingine anaenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli. 33Ninyi mlituma watu kwa Yohana, akaishuhudia kweli. 34Lakini mimi sipokei ushuhuda kwa wana Adamu; walakini ninasema haya illi ninyi mpate kuokoka. 35Yeye alikuwa taa iwakayo na kuangaza, na ninyi mlipenda kuishangilia nuru yake kitambo. 36Lakini ushuhuda nilio nao ni mkubwa kuliko ule wa Yohana: kwa kuwa zile kazi nilizopewa na Baba nizimalize, kazi hizo zenyeye ninazozitenda zinanishuhudia kwamba Baba amenituma. 37Nae Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona. 38Na neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hamwamini yeye alivetumwa nae. 39Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yanayonishuhudia: 40wala hamtaki kuja kwangu, mpate kuwa na uzima. 41Sipokei utukufu kwa wana Adamu. 42Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu. 43Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei: mwingine akija kwa jina lake mwenyewe mtampokea huyo. 44Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokezanya utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti? 45Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba: yuko anaewashitaki, yaani Musa, mnaemtumaini ninyi. 46Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; maana yeye aliandika khahari zangu. 47Illakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaaminije maneno yangu?
موجودہ انتخاب:
Yohana MT. 5: SWZZB1921
سرخی
شئیر
کاپی
کیا آپ جاہتے ہیں کہ آپ کی سرکیاں آپ کی devices پر محفوظ ہوں؟ Sign up or sign in
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.