Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuihesabu gharama kama ana vitu vya kuumaliza? Asije akawa hawezi kuumaliza baada ya kuweka msingi, watu wote wakaanza kumdhihaki, wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.