Yn 7

7
Kutoamini kwa Ndugu za Yesu
1 # Mk 9:30; Lk 9:51 Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Uyahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua. 2#Law 23:34; Kum 16:13Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu. 3#Yn 2:12; Mt 12:46; Mdo 1:14Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. 4Kwa maana hakuna mtu afanyaye neno kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhihirishe kwa ulimwengu. 5#Mt 13:55Maana hata nduguze hawakumwamini. 6#Yn 2:4Basi Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote upo. 7#Yn 15:18Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. 8Kweeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sikwei bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa haujatimia wakati wangu. 9Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alikaa vivi hivi huko Galilaya.
Yesu katika Sikukuu ya Vibanda
10Hata ndugu zake walipokwisha kukwea kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipokwea, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri. 11Basi Wayahudi wakamtafuta kwenye sikukuu, wakasema, Yuko wapi yule? 12Kukawa na manung’uniko mengi katika makutano juu yake. Wengine wakasema, Ni mtu mwema. Na wengine wakasema, Sivyo; bali anawadanganya makutano. 13#Yn 9:22; 12:42; 19:38Walakini hakuna mtu aliyemtaja waziwazi, kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi.
14Hata ikawa katikati ya sikukuu Yesu alikwea kuingia hekaluni, akafundisha. 15#Mt 13:54; Lk 2:47Wayahudi wakastaajabu wakisema, Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma? 16#Yn 12:49Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka. 17Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. 18#Yn 5:41,44Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anayetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu. 19#Yn 5:16,18,47; Mdo 7:53; Rum 2:17-29Je! Musa hakuwapa torati? Wala hakuna mmoja wenu aitendaye torati. Mbona mnatafuta kuniua? 20#Mk 3:21; Yn 8:48,52; 10:20Mkutano wakajibu, Ama! Una pepo! Ni nani anayetafuta kukuua? 21#Yn 5:16Yesu akajibu, akawaambia, Mimi nalitenda kazi moja, nanyi nyote mnaistaajabia. 22#Mwa 17:10; Law 12:3Musa aliwapa tohara; lakini si kwamba yatoka kwa Musa, bali kwa mababa; nanyi siku ya sabato humtahiri mtu. 23#Yn 5:9Basi ikiwa mtu hupashwa tohara siku ya sabato, ili torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia mimi kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato? 24#Yn 8:15Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.
Huyu ndiye Kristo?
25 # Yn 7:19 Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue? 26Na kumbe! Anena waziwazi, wala hawamwambii neno! Yamkini hao wakuu wanajua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo? 27#Yn 7:41Lakini huyu twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako. 28Basi Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. 29#Mt 11:27Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma. 30#Yn 8:20; 13:1; Lk 22:53Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado. 31#Yn 8:30; 10:42; 11:45; 12:42Na watu wengi katika mkutano wakamwamini; wakasema, Atakapokuja Kristo, je! Atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu?
Maofisa Watumwa Kumkamata Yesu
32Mafarisayo wakawasikia mkutano wakinung’unika hivi juu yake; basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma watumishi ili wamkamate.
33 # Yn 13:33 Basi Yesu akasema, Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; kisha naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka. 34#Yn 8:21; 13:36; 17:24Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja. 35Basi Wayahudi wakasemezana, Huyu atakwenda wapi hata sisi tusimwone? Ati! Atakwenda kwa Utawanyiko wa Wayunani, na kuwafundisha Wayunani? 36Ni neno gani hilo alilolisema, Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja?
Mito ya Maji yaliyo Hai
37 # Law 23:36; Yn 4:10,14 Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. 38#Eze 47:1,12; Zek 13:1; 14:8; Yoe 2:28; 3:18; Isa 44:3; 55:1; 58:11Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. 39#Yn 16:7; 2 Kor 3:17Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.
Mgawanyiko kati ya Watu
40 # Yn 6:14; Kum 18:15 Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule. 41#Yn 1:46Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo. Wengine wakasema, Je! Kristo atoka Galilaya? 42#2 Sam 7:12; Mik 5:2; Mt 2:5,6; 22:42; Zab 89:3Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi? 43#Yn 9:16Basi kukaingia matengano katika mkutano kwa ajili yake. 44#Yn 7:30Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hakuna mtu aliyenyosha mikono yake ili kumshika.
Kutoamini kwa wenye Mamlaka
45 # Yn 7:32 Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta? 46#Mt 7:28,29Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena. 47Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika? 48#Yn 12:42Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo? 49Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa. 50#Yn 3:1-2Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao), 51#Kum 1:16,17; 19:15Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo? 52#Yn 1:46; 7:41Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya! Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.

Айни замон обунашуда:

Yn 7: SUV

Лаҳзаҳои махсус

Паҳн кунед

Нусха

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in