Mwanzo 10
10
Mataifa Yaliyotokana Na Noa
(1 Nyakati 1:5-23)
1 Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.
Wazao Wa Yafethi
2 Wana wa Yafethi walikuwa:
Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
3 Wana wa Gomeri walikuwa:
Ashkenazi, Rifathi na Togarma.
4 Wana wa Yavani walikuwa:
Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. 5(Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.)
Wazao Wa Hamu
6 Wana wa Hamu walikuwa:
Kushi, Misraimu,#10:6 Yaani Misri. Putu na Kanaani.
7 Wana wa Kushi walikuwa:
Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.
Wana wa Raama walikuwa:
Sheba na Dedani.
8 Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani. 9 Alikuwa mwindaji hodari mbele za Bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za Bwana.” 10 Vituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari. 11 Kutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala, 12na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.
13Misraimu alikuwa baba wa:
Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, 14 Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.
15 Kanaani alikuwa baba wa:
Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi, 16 Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, 17 Wahivi, Waariki, Wasini, 18 Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.
Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika, 19 na mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.
20Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.
Wazao Wa Shemu
21 Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.
22 Wana wa Shemu walikuwa:
Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
23 Wana wa Aramu walikuwa:
Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
24 Arfaksadi alikuwa baba wa Shela,
naye Shela akamzaa Eberi.
25Eberi akapata wana wawili:
Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake ndipo dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.
26Yoktani alikuwa baba wa:
Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 27 Hadoramu, Uzali, Dikla, 28 Obali, Abimaeli, Sheba, 29 Ofiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.
30Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki.
31Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.
32Hizi ndizo koo za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.
தற்சமயம் தேர்ந்தெடுக்கப்பட்டது:
Mwanzo 10: NEN
சிறப்புக்கூறு
பகிர்
நகல்
உங்கள் எல்லா சாதனங்களிலும் உங்கள் சிறப்பம்சங்கள் சேமிக்கப்பட வேண்டுமா? பதிவு செய்யவும் அல்லது உள்நுழையவும்
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.
Used with Permission. All Rights Reserved Worldwide.