Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

SIKU 1 YA 28

Mwandishi ni mfalme Daudi. Anamhimidi Bwana kwa sababu ameona fadhili zake maishani mwake. Ni jinsi fadhili za Bwana zilivyo, zinawalenga watu, mtu mmoja mmoja. Ni kwa ajili ya kuwapatia watu mema:Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai(m.4-5). Anakusamehe maovu yakoyote, kupona kwako kunatoka kwake pia, na anakupa uhai unaoshinda hata kaburi. Unashibishwa na mema, na yote yanatoka kwa Bwana. Jambo kuu katika mistari hii ni:Mungu ni mtoaji wa mema yotenawewe ni mpokeaji wa mema yote. Kwa hiyo:Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/2025

Soma Biblia Kila Siku 02/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Zaburi na Isaya. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz