Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Msingi Wa Mungu UsiotikisikaMfano

Msingi Wa Mungu Usiotikisika

SIKU 3 YA 4

Naweza Kumwamini Mungu Wangu Asiyetikisika

‘Njoni myatazame matendo ya Bwana, jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.’ – Zaburi 46:8

Mwandishi wa Zaburi 46 anatuhimiza tukumbuke kile ambacho Mungu amefanya na, kama tunavyokumbuka, kujifunza kumwamini Mungu katika maisha yetu yajayo.

Watu wa Israeli waliacha nafasi katika maisha yao ili kukumbuka, akilini njia ambazo Mungu ameingilia kati katika historia kwa ajili ya mema yao (Kumbukumbu la Torati 26:5-11). Ilikuwa kipengele cha kati cha ibada yao na kilitoa utambulisho wao. Kumwamini Mungu aliyetoa kwa ajili ya mahitaji ya watu, anayejitokeza na kutoa wokovu, kueneza Agano la Kale na kufikia utimillifu katika Agano Jipya kupitia kwa kazi ya kuokoa ya Yesu.

Unaweza kukumbuka kwamba Yesu, Mungu katika hali ya mwanadamu analeta uhakika. Yesu anafahamu kuwa na furaha maana yake nini na maumivu ya moyo, kulia na kucheka na huzuni. Anafahamu maana yake nini kuchoka, kuwa na njaa na kusherehekea.

Tunapokuja mbele zake Mungu, hatuhitaji kuja na kilichosafishwa, tolea la maneno sahihi yaliyo moyoni. Yesu anafahamu inafananaje kuwa mwanadamu. Tunakuja kwa ukweli kama tuwezavyo, tukifahamu kwamba anatusikia na kutuelewa.

Kutafakari:

Chukua muda utafakari kuhusu maisha yako. Unaweza kuchagua kuyagawa katika miongo au nyakati maalum. Kumbuka nyakati ambazo ulitambua uwepo wa Mungu.

Kumbuka yale ambayo Mungu amekutendea ndani na kwa ajili yako.

Unaweza kujifunza nini kutokana na haya kinachoweza kuleta uhakika kwa wakati uliopo na wakati ujao?

Maombi:

Mpendwa Bwana, ninavyokumbuka uaminifu wako kwangu huko nyuma, napata uhakika wa msaada wako na wokovu. Asante kwamba hali yangu ya sasa sio kwamba haijulikani kwako. Wewe ndiye Mungu asiyetikisika, nami naweka tumaini langu kwako.

Amina.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Msingi Wa Mungu Usiotikisika

Tunapofikiria hali ya dunia tunayoishi ndani yake, mahali vita na migogoro vinaonekana kutawala kila kituo cha habari, majanga ya asili yanawakumba watu duniani na mahali ambapo mahusiano yaliyo vunjika ni ya kawaida ndani ya jamii, tunatazama Zaburi 46, inayotupa ujasiri kwamba Mungu ndiye msingi usiotikisika katika mazingira yoyote. Tunabadilika, mazingira yetu yanabadilika, lakini Mungu wetu habadiliki.

More

Tungependa kumshukuru The Salvation Army International kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org