Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

NuruMfano

Nuru

SIKU 3 YA 5

Kuwa Nuru Kama Balozi

Hakuna mtu katika historia ambaye amemwakilisha Mungu kwa ukamilifu zaidi kuliko Kristo. Kupitia kwake, watu wangeweza kuupata ukarimu wa Mungu, uwepo wake, na upendo wake. Yesu ni mwakilishi kamili wa tabia ya Mungu na nia zake kwa wanadamu. Kuzingatia jinsi Yesu alivyomwakilisha Mungu kwa dunia kwa ukamilifu, ni ajabu kufikiria jinsi Yesu anavyowaita watu wa kawaida walio na mapungufu kama wewe na mimi kuwa wawakilishi wake. Yesu hakujua dhambi. Hakuutafuta ustawi wake mwenyewe. Aliishi kwa huduma kwa wengine na kwa maneno na matendo yake alitoa ujumbe uliouakisi moyo wa Mungu kwa ukamilifu.

Paulo aliliandikia kundi la kwanza la waumini, akiwaasa na kuwapa changamoto kuelewa jinsi sisi sote tunaomfuata Yesu ni mabalozi wake. Kama mabalozi waliotumwa kutoka nchi yao, tunapaswa kujiona kuwa tumetumwa nje kuwakilisha ufalme wa Kristo, maadili yake, na ujumbe wake. Yeyote anayekutana na balozi wa taifa jingine pia anapaswa kuelewa taifa letu linahusu nini. Tumeeleza jinsi unapoamini na kumtumaini Yesu, unakombolewa kutoka ufalme wa giza na kurejeshwa kwenye ufalme chini ya utawala wa upendo wa Kristo (Wakolosai 1:13). Kwa njia ile ile ambayo watu wangeweza kujifunza kuhusu ufalme huu walipokutana na Yesu, una nafasi ya kuwaonyesha na kuwafundisha watu unaokutana nao kuhusu Mfalme wa upendo, Yesu.

Hata na vitu vizuri duniani vinavyoakisi ufalme wa Mungu, bado vinaakisi mahali pasipotambua Yesu kama Bwana na matokeo yake ni kuwa kumejaa uharibifu.

Lakini waumini ni wa Mfalme ambaye utawala wake ni mzuri na anayetaka mema kwa ajili yetu. Tunaishi kila siku kati ya watu na mahali pasipotambua Yesu kama Mfalme mzuri ambaye ni yeye—mtu ambaye anafaa kujiwasilisha kikamilifu na kutumaini mamlaka yake. Unapoishi na Kristo kama Mfalme wako, unawakilisha nchi/ufalme wa kweli unaotoka.

Fikiria ni kitu gani wengine wanaweza kuona na kujifunza kuhusu nchi yako ya mbinguni kwa kukuangalia. Ni nini muhimu zaidi pale? Nani ni muhimu zaidi pale? Je, maisha yako yanawakilisha amani, upendo, furaha, na tumaini alizoonyesha Yesu ambazo zilifichua ufalme wake kwa wengine?

Sala

“Mungu, nisaidie kukuakilisha wewe na ujumbe wako vizuri kama balozi wako duniani.”

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Nuru

Yesu anatueleza katika Agizo Kuu kwamba tunapaswa kwenda na kufanya wanafunzi wa mataifa yote. Lakini mfuasi wa Yesu hufanya wanafunzi vipi? Mpango huu wa usomaji unatoa mfumo wa kibiblia wa jinsi waumini wanavyofundisha wengine kutii kila kitu Yesu alichoamuru, katika kutembea kwao binafsi na Yeye na pamoja na jamii ya waumini.

More

Tungependa kumshukuru Who am I? kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://whoamitoyou.com?lng=sw