Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

MzabibuMfano

Mzabibu

SIKU 11 YA 12

Kuhudumiana

Dunia ambayo kanisa la kwanza lilianza kukua inaweza kuwa katili. Roma ambayo ilimiliki maeneo mengi ambapo injili ilikuwa imeenea haikuweka thamani kubwa kwa maisha yote ya binadamu. Wanawake, watoto na watu wa tabaka za chini wangeweza kutendewa kama mali. Lengo la watu wengi lilikuwa kupanda katika hali ya kijamii ambayo ina maana walikuwa wakiendelea kufuata maslahi yao wenyewe kwa gharama za wengine.

Hiyo ni sababu moja kwa nini utamaduni huu wa ushindani haukuweza kuelewa kanisa la kwanza. Wafuasi wa Yesu waliishi tofauti kabisa wakiiga Kristo katika huduma yake kwa kila mtu. Yesu alifanya majukumu ya mtumishi kuonyesha upendo na kujitolea kwake kwa wafuasi wake (Yohana 13:1-17). Hata zaidi ya kushangaza Aliweka kando utukufu na hadhi yake kuwa mwanadamu wa hali ya chini na mwishowe kufa kifo cha aibu zaidi (Wafilipi 2:5-8).

Kwa mfano wa Yesu na kwa sababu hali yao na kukubalika mbele ya Kristo hakuweza kubadilika, kanisa liliachiliwa kutoka kwa shinikizo la kitamaduni la kujikweza. Badala yake walikuwa huru kuwahudumia wengine. Mtume Paulo aliwaagiza hivi: "Msifanye chochote kwa nia ya ubinafsi au majivuno. Bali kwa unyenyekevu waheshimuni wengine kuliko nafsi zenu, kila mmoja akitazama maslahi ya wengine wala siyo yake mwenyewe" (Wafilipi 2:3-4).

Inawezekana je "kuheshimu wengine zaidi ya nafsi yako" kubadilisha maisha yako - jinsi unavyotumia muda wako, jinsi unavyokaribia mahusiano, jinsi unavyojiangalia mwenyewe? Ikiwa unaweza kukusanyika na waumini wengine, kuhudumiana kunaonekanaje katika maisha ya kila siku? Ni hatua ndogo gani unaweza kuchukua kuiga moyo wa huduma wa Kristo kwa mtu? Fikiria kutumia sala iliyo hapa chini kuanza.

Sala

"Mungu nakiri kwamba wakati mwingine ni rahisi sana kutenda ubinafsi na familia na marafiki zangu. Nahitaji msaada wako kuweka wengine mbele yangu mwenyewe. Nionyeshe jinsi hiyo inavyoonekana leo. Asante kwamba sina haja ya kupata au kujitahidi kwa hali yoyote na Wewe."

Chunguza Kwa Kasi Yako

Inaweza kuwa rahisi kuhudumia watu unaowapenda. Lakini iweje kuhusu watu ambao ni wagumu? Au watu wanaokuchukia? Soma Warumi 12:9-21 na fikiria himizo la Paulo kwa Wakristo katika jiji la Roma ambao wangeweza kukumbana na mateso makubwa kwa sababu ya imani yao.

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Mzabibu

Moja ya maswali ya kawaida kwa watu ambao ni wapya katika kumfuata Yesu ni, “Nifanye nini sasa?” Ina maana gani kumpenda, kumtii, na kuwa sehemu ya jamii ya waumini? Mpango huu wa usomaji unatoa mfumo wa kibiblia wa jinsi ya kuunganisha uhusiano wako wa kibinafsi na Yesu na utume wa kanisa.

More

Tungependa kumshukuru Who am I? kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://whoamitoyou.com?lng=sw