Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuanza: Mwongozo Rahisi Wa Kuomba Kwa UjasiriMfano

Kuanza: Mwongozo Rahisi Wa Kuomba Kwa Ujasiri

SIKU 1 YA 6

Maombi ni Kipaumbele

Katika Mathayo 9:37–38, Yesu alisema "Mavuno ni mengi, lakini watendakazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno, atume wafanya kazi katika mavuno yake (CSB, msisitizo umeongezwa).”

Neno "kutuma" katika Kigiriki linamaanisha "kusukuma". Propel Women ilianzishwa kwa msingi wa msitari huu. Kwa hivyo tunapotafuta kuanza maombi yetu, tutafanya kile ambacho Yesu aliamuru: tutamwomba Bwana wa mavuno atume wafanyakazi—kutusukuma—katika mavuno yake. Mavuno ni mengi. Fursa ya Ufalme wa Mungu kusonga mbele iko hapa sasa. Ni nini ufunguo wa kuuona ukitokea? Maombi!

Maombi yanamaanisha kuzungumza na Mungu. Yanaweza kuwa mazungumzo yanayotokea moyoni mwako au kwa sauti. Yanaweza kutokea ukiwa peke yako au katika kikundi. Yanaweza kutokea miguu yetu ikiwa imesimama imara juu ya ardhi, au maelfu ya futi juu angani. Lakini hapa kuna jambo la kushangaza: Tunapoomba, Mungu anasikiliza, ananena, na anajibu.

Mungu wa Ulimwengu anataka kusikia kutoka kwako. Mungu hajaanzisha tu mazungumzo na kutualika tuzungumze naye katika maombi, bali pia anaunganisha maombi yetu katika kazi anazofanya ulimwenguni!

Popote ulipo, uwe umetoka wapi, bila kujali eneo lako la kazi – katika soko, kama mama anayekaa nyumbani, Mkurugenzi Mtendaji, daktari, mwalimu, mwanasheria, au msanii - maombi ni mahali pa msingi ambapo kazi ya Mungu na kazi yako katika ulimwengu huu hukutana. Tunapoomba, Mungu ameahidi kuhamisha milima, kutikisa misingi na kufikia mavuno mengi ya watu ambao bado hawajamjua. Mungu amefanya iwe kwamba maombi yetu madogo yanaleta tofauti ya milele na yenye ukubwa wa Ufalme! Mungu anabadilisha ulimwengu kwa nguvu zake na kupitia maombi yetu!

Sala

"Bwana, naomba kwamba huu ni mwaka ninaokuona ukienda kwa nguvu ili kuleta watu kwako. Kwa mujibu wa Neno lako katika Mathayo 9:37-38, na kuwe na wafanyakazi wengi zaidi wanaosukumwa kwenye mavuno kuliko wakati mwingine wowote. Siku zijazo ziwe na mavuno makubwa kwa utukufu wako na maendeleo ya Ufalme Wako hapa duniani. Na ninajikabidhi kwako sasa kwamba nitakuwa sehemu yake. Amina."

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Kuanza: Mwongozo Rahisi Wa Kuomba Kwa Ujasiri

Maombi ni zawadi, fursa nzuri ya kuwa na uhusiano na Baba yetu wa Mbinguni. Katika mpango huu wa siku 6, tutatambua yale ambayo Yesu alitufundisha kuhusu maombi na kuhimizwa kuomba kwa mfululizo na ujasiri mkubwa.

More

Tungependa kuwashukuru Christine Caine - A21, Propel, CCM kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.propelwomen.org/