Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

SIKU 4 YA 31

Yesu alizaliwa, Mfalme Herode alipotawala. Mamajusi walikuwa watu wenye hekima; walifika Yerusalemu wakiongozwa na nyota. Walimwuliza Mfalme Herode, Yuko wapi Mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa? Herode alifadhaika sana na maelezo yao. Alifikiri ananyang’anywa ufalme, akaanza kuhangaika akiita watu maarufu ili awaulize,Kristo azaliwa wapi?"Kristo", maana yake ni "mpakwa mafuta wa Bwana". Yaani Yesu ni Mfalme aliyepewa kutimiza unabii wa Isaya 9:6-7,Kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Tafakari pia Yesu anavyoeleza katika Yn 18:36-37 kuelewa ufalme wake ulivyo,Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/