Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

SIKU 27 YA 31

Tunaposingiziwa kwa mambo tusiyoyatenda inauma sana. Ndivyo ilivyompata Dauti. Analalamika kwa kusingiziwa mambo ya uongo toka kwa maadui zake. Katika mazingira hayo, bado Daudi anaweka mategemea yako kwa Mungu na kuamini kuwa Mungu hatawaruhusu maadui zake wapate ushindi juu yake. Daudi anaona vema kwamba badala ya kutumia kinywa chake kuwalaumu maadui zake, yeye atumie midomo na kinywa chake kueleza sifa na haki ya Mungu. Ombi lake kubwa ni kwamba uovu ushindwe na haki ipate ushindi (m.26-28,Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja, Wanaoifurahia hali yangu mbaya. Wavikwe aibu na fedheha, Wanaojikuza juu yangu. Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe Bwana, Apendezwaye na amani ya mtumishi wake. Na ulimi wangu utanena haki yako, Na sifa zako mchana kutwa).

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2024

Soma Biblia Kila Siku 01/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/