Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

SIKU 29 YA 30

Kukasirika si dhambi. Lakini kuna hasira itendayo dhambi. Hasira isiyotenda dhambi ni ile ichukiayo uovu utendwao katika jamii. Uteteapo Neno la Mungu kwa kukemea uovu, usiogope watu wala vyeo au nafasi walizo nazo katika jamii, maana ni kujitega mwenyewe. Bali umwogope Mungu na kuongozwa naye. Ukiwa na hofu juu ya Mungu unajenga heshima, kutegemea, imani na utii. Kumwogopa Mungu kunaleta ulinzi dhidi ya wanaokusudia kukudhuru, u salama:Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; bali amtumainiye Bwana atakuwa salama(m.25). Linganisha na Mwa 50:18-20 na 1 Pet 5:5-6:Nduguze [Yusufu] wakaenda tena, wakamwangukia miguu, wakasema, Tazama, sisi tu watumwa wako.Yusufu akawaambia, Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu?Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo. ... Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake.

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Warumi na Methali. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/