Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

SIKU 3 YA 31

Sisi wanadamu tunatoa hukumu zisizo za haki kwa wengine, kwa sababu tunajali tu matakwa yetu. Lakini Bwana Yesu alitenda kazi kwa njia tofauti. Hutoa hukumu za haki. Unajua ni kwa sababu gani? Zingatia m.30 unaosema,Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka. Pia twapenda kujisifu na kujitangaza. Lakini Yesu je? Yeye hufanya tofauti. Hajishuhudii! Lakini ushuhuda wa Yohana Mbatizaji, Maandiko Matakatifu na kazi afanyazo zinamshudia Yesu kwa sauti moja kuwa Kristo. Hivyo usiwe na wasiwasi kumwamini. Ndiyo kupata uzima wa milele.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/