Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

SIKU 29 YA 31

Usinipe umaskini wala utajiri” (m.8). Ni ombi lenye hekima, maana umaskini na hasa utajiri unaweza kuwa kiini cha watu kumwacha Mungu. Utajiri si jibu la kila kitu. Kuwa tajiri wa mali kunahatarisha maisha ya kiroho. Yesu anaonya akisema,Amin, nawaambieni, ya kwamba itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. Nawaambia tena, Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu(Mt 19:23-24). Vivyo hivyo kuwa maskini wa mali kunahatarisha roho na mwili pia. Tukiwa na vingi ama kidogo, tujifunze kuishi kwa kuridhika na kutosheka. Paulo anasisitiza kuwasi kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu(Flp 4:11-13). Utoshelevu wa kweli na hakika ni kukaa pamoja na Mungu, Muumba na Mwokozi wako.

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/