Kubaki Katika KristoMfano
Ibada ya Siku ya Pili
Maana ya Kubaki Ndani ya Kristo
Katika kifungu cha tatu, Kristo anawaambia wanafunzi wake kuwa tayari ni wasafi. Alikuwa ameshawaambia hivyo katika Yohana 13:10, alipowasafisha miguu kabla ya kukaa mezani na kushiriki Mlo wa Bwana wa Jioni katika Chumba cha Juu. Hapo katika Yohana 13:10, hivi ndivyo alivyowaambia: Nyie ni wasafi ingawa siyo kila mmoja wenu.
Kristo aliposema, siyo kila mmoja wenu, alimaanisha Yudasi Iskariote ambaye alipanga njama ya kumsaliti. Kwa hivyo hili neno usafi alilolitumia Kristo linamaanisha wale wasiofanana na Yudasi Iskariote kwa sababu imani yao na kujitolea kimungu katika Kristo ni ya dhati.
Kwa hiyo Kristo anapotumia usemi wa kukaa au kubaki ndani yake anamaanisha kwanza kabisa kutubu dhambi zetu, kuiweka Imani yetu katika kile kitendo alichotutendea msalabani, ili tuunganishwe naye kiroho kama vile matawi yanavyoungana na mzabibu.
Neno la awali la Kigiriki lililotafsiriwa kwa kiingereza kama Kubaki ndani katika kifungu hiki, linamaanisha kukaa, kudumu, kuishi, kustahimili, na kuendelea. Kwa hivyo, Kristo anasema hivi, tujapo mbele zake kwa Imani, twaja ili kukaa, kudumu, na kuendelea kuishi naye katika hali za aina zote.
Katika kifungu cha pili, Kristo anaeleza kwamba baba yake anakata kila tawi lisilozaa matunda. Yudasi ni kielelezo au mfano wa tawi lililokatwa kwa sababu ya kutoweka imani yake kwa Kristo, na kutojitolea kimungu kwa dhati.
Msiba uliompata Yudasi unatuonyesha ole kwao wote wanaojihusisha na makanisa lakini sio wakristo kwa sababu hawajatubu dhambi na kuweka imani yao ndani ya kazi aliyotutimizia Kristo pale msalabani ili wapate kuanza kuishi, kudumu na kuendelea na maisha ya kiroho ndani ya Kristo.
Katika kifungu cha pili, Kristo anaeleza kwamba matawi yaliyomo ndani yake yanayozaa matunda yatapogolewa ili kuongeza mazao zaidi.
Kupogolewa kwa mizabibu iliyo na afya ni muhimu kwa sababu mzabibu usiyopunguzwa hunawiri lakini mazao yake ni duni kwa sababu utomvu mwingi unatumika kukuza matawi na siyo zabibu.
Katika kifungu hiki, Kristo anaeleza kwamba Baba yetu wa Mbinguni ndiye Mkulima au mtunza bustani naye hutumia au hurusu mambo magumu maishani mwetu ya Ukristo ili kupunguza na kupogoa kimwili ili tuweze kuzaa matunda zaidi ya kiroho na kukomaa kiroho.
Kwa hivyo, muhtasari wa somo letu ni kwamba maana ya usemi huu, kukaa au kubaki ndani ya Kristo ni kwa kupitia kutubu dhambi na kuweka imani yetu kwa kazi aliyotutendea Kristo pale msalabani, ili tuunganishwe naye kama vile ilivyo muhimu kwa uhai wa matawi ya mizabibu kuunganishwa na mzabibu. Hivi ndivyo mfumo wa kubaki ndani ya Kristo unavyoanza maishani mwetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Katika kifungu hiki, kwanza, Kristo anatuwezesha kuelewa maana ya kubaki ndani yake. Pili, Kristo anatuwezesha kuelewa taratibu zinazochangia kuimarisha kubaki au kukaa ndani yake. Tatu, Kristo, anafafanua alama tatu zinazotutambulisha kama tupo ndani yake.
More
Tungependa kuwashukuru Emmanuel Kwasi Amoafo kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://returningtothegospel.com/