Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

SIKU 21 YA 31

Huko Ashdodi na Misri walikaa watu wa mataifa wasiokuwa na ufahamu wa Mungu kama Waisraeli. Lakini katika m.9 wanaitwa watazame udhalimu wa watu wa Mungu na hukumu yake juu yao:Tangazeni habari katika majumba ya Ashdodi, na katika majumba ya nchi ya Misri, mkaseme, Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria, katazameni, ni mishindo mikubwa kama nini iliyomo humo, na udhalimu mwingi kama nini uliomo ndani yake. Wasamaria wote wamefanana, kwa kukandamiza na kuwaonea wanyonge. Wema haufahamiki kwao hawa! Kwa hiyo Mungu atainua maadui wawe fimbo yake ya kuwapiga watenda mabaya.Hapana amani kwa wabaya, asema Bwana(Isa 48:22). Maneno haya ni kwa watu wote, kwangu na kwako, ili tuache kutenda mabaya mbele za Mungu apendaye haki.

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023

Soma Biblia Kila Siku Julai 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Kutoka na Amosi Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/