Siku Sita Za Majina Ya MunguMfano
SIKU YA 3: JEHOVAH JIREH – BWANA ATATOA
Huna uhakika wa jinsi utakavyolipa mahitaji yako mwezi huu. Hali ya uhusiano wako iko hewani. Umesikia kwamba kupunguzwa kwa kazi kunakuja kazini, na hauna uhakika kuhusu wadhfa wako katika kampuni. Mambo ya msingi ya maisha yanapokuwa hatarini—afya, fedha, makao, chakula, familia, kazi ya kuajiriwa—ni jambo la kawaida kuogopa, kana kwamba huna pa kuelekea. Hapo ndipo unapohitaji kumwita Jehovah Jireh. Jina hili lililobarikiwa la Mungu linamaanisha “Bwana atatoa,” na ni jina lililojaa nguvu na uweza.
Tunapohisi hofu kuhusu maisha yetu yajayo, ni muhimu kumgeukia Mungu na kuliitia jina lake. Kila zawadi nzuri na kamilifu hutoka kwake, na hakuna kikomo kwa karama na baraka anazotoa. Kuweka imani yetu kwake wakati mwingine kunaweza kuwa njia pekee ya kutuliza woga wetu na kudumisha mawazo mazuri yenye matarajio au kuwa chanya.
Inaweza kuwa somo gumu kujifunza, lakini majaribu hapa duniani huimarisha misuli yetu ya kiroho na kutuvuta karibu na Mungu. Kupitia mapambano yetu, anatuonyesha moja kwa moja jinsi anavyotoa hewa kwa mapafu yetu kupumua na mwanga kwa macho yetu kuona. Anatupa kile hasa tunachohitaji ili kuzalisha ukuaji mkubwa ndani yetu na athari inayofikia mbali zaidi kwa ufalme wake. Na daima huitoa kwa roho ya upendo.
Kuhusu Mpango huu
Kutoka kwa majina mengi aliyo nayo Mungu, Yeye ametufunulia vipengele vya tabia yake na asili yake. Zaidi ya majina haya ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Biblia inaonyesha majina zaidi ya 80 tofauti ya Mungu. Hapa kuna majina sita na maana zake ili kumsaidia muumini kumkaribia Mungu Mmoja wa Kweli. Hii ni dondoo kutoka kwa kitabu cha Uzoefu wa Nguvu ya Majina ya Mungu: Ibada itoayo Maisha ya Kuishi na Dk. Tony Evans.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/