Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuhama Kutoka Kwenye Kuvunjika Kuelekea KusudiMfano

Kuhama Kutoka Kwenye Kuvunjika Kuelekea Kusudi

SIKU 3 YA 3

Watu wengi leo wanakosa majibu wanayohitaji kuhusu jinsi ya kushughulikia matatizo katika maisha yao. Zaidi ya hayo, wanakosa uhakikisho wa imani kwamba – kile kinachoonekana kuwa kimevunjika katika maisha, nyumba, na taifa lao kinaweza kurejeshwa. Labda ni ndoa iliyovunjika. Labda kazi iliyofikia mwisho. Inaweza kuwa fikra mbaya. Chochote ambacho kimesababisha Wakristo wengi kulala chini na kulegea kinaonekana kuwa kimenyonya tumaini la suluhu pia.

Ikiwa ni wewe, kumbuka kuwa ni vigumu kurekebisha tatizo wakati hujui, au chagua kupuuza sababisho. Matumaini yanaondoka tunapozingatia dalili na sio madhambi yaliyoleta hizo dalili. Wakati wowote unapotafuta tiba, lazima ushughulikie sababu. Kwa muda mrefu, watu wengi wa kawaida katika makanisa, wachungaji, na wanasiasa wanazingatia dalili badala ya kushughulikia mizizi ya kimfumo ambayo imesababisha uozo. Iwapo tutawahi kurekebisha maisha yetu, nyumba zetu, makanisa na taifa, inatubidi kushughulikia mambo ya kiroho chini ya uvunjifu tunaouona.

Je, kuna eneo katika maisha yako ambapo umejizuia kutambua chanzo cha matatizo yanayokukabili, ambayo yamekuzuia ama kuyaponya au kuyashinda?

Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Kuhama Kutoka Kwenye Kuvunjika Kuelekea Kusudi

Uwe nani, Mungu ana kusudi na mpango wa maisha yako. Wakati mwingine tunakwama katika kuvunjika kwetu na kupoteza matumaini kwamba tutagundua njia ya Mungu kwa maisha yetu. Kama mwandishi ambaye vitabu vyake vinauzwa san...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha