Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Msalaba Na PasakaMfano

Msalaba Na Pasaka

SIKU 1 YA 7

Tambulisho Letu na Tumaini Letu

Katika kuwaandikia wasikilizaji wake huko Galatia, Paulo aliwahimiza tena na tena, kwa namna moja au nyingine, wamkumbuke Kristo na msalaba. Paulo alipokuwa anamalizia barua yake kwa Wagalatia, alifanya yale ambayo mara nyingi tutafanya leo kwa kutumia maandishi ya mlalo, kupigia mstari chini ya herufi, kufanya herufi kuwa kubwa, kuongeza rangi zaidi kwa maandishi, au kwa njia zozote zile, alisisitizia mada yake kwa kuandika kwa maandishi makubwa. Kimsingi Paulo alisema, “Sitaki ukose sehemu hii. Sikiliza na usome kwa makini.”

Inasema kwamba Paulo aliandika kwa “herufi kubwa” kwa mkono wake mwenyewe (Wagalatia 6:11) ili kuwaambia wasikilizaji wake kwamba yeye ndiye anayeandika, na kwamba ukweli aliokuwa akiwaambia ulitoka kwenye chanzo kimoja. Aliandika katika mstari wa 14, “Lakini mimi mwenyewe nisione fahari juu ya kitu chochote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulubishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.”

Paulo alikuwa ameokolewa kwa muda, na bado alikuwa akisema, "Nitajisifu tu juu ya msalaba." Hakuruhusu ukweli wa kihistoria wa msalaba kupoteza umuhimu wake wa kisasa. Jambo pekee la Paulo alilorejelea katika maisha yake lilikuwa msalaba. Msalaba ulikuwa kitovu cha kuwepo kwake. Msalaba ulikuwa hewa ya pumzi yake, mpigo wa moyo wake na kiini cha umuhimu wake. Ilikuwa ni nguvu ya kushinda udhaifu wake.

Sala: Baba, nisijisifu kamwe kwa nguvu zangu au kwa uwezo wangu mwenyewe. Ni msalaba wa Yesu Kristo ambao umefanya maisha yangu yawezekane - ni kwa nguvu zake kwamba nimepata faida yangu binafsi. Chochote kizuri nilichonacho ni zawadi inayoshuka kutoka Kwako Bwana, kutoka kwa moyo wako wa rehema kupitia Kristo aliyesulubiwa katika jina la Kristo, amina.

Mtafute Yeye, Watumikie Wengine

Andika kumbukumbu leo ​​ili kuonyesha thamani kwa mtu au watu wengi unaokutana nao. Watendee kwa hadhi ambayo Kristo alikufa ili kuwapa na kisha chukua muda kutoka kwenye masaa yako kumtumikia mtu mwingine kwa moyo wa shukrani.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Msalaba Na Pasaka

Tunavaa misalaba shingoni mwetu, lakini tunapaswa kuitumiaje kwa maisha yetu? Kazi ya Yesu ina nguvu ya ajabu kwetu. Bila Ijumaa, hakungekuwa na Jumapili. Pasaka isingetokea bila msalaba. Gundua jinsi msalaba unavyounganamanisha katika maisha yako kupitia mpango huu wa usomaji wa ibada unapotayarisha moyo wako kwa Pasaka.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/