Fukuza HofuMfano
Je, umewahi kupanda ndege kupitia misukosuko mikali? Huenda ndege ilionekana kutokuwa na udhibiti kwa muda, na pengine uliingiwa na woga kidogo. Ikiwa mkanda wako wa kiti ulikuwa umeufunga tayari, huenda uliukaza zaidi. Pengine ulishikilia kiti chako kwa nguvu kidogo. Huenda ulihisi kutotulia kwa sababu ulininginia kwa muda hewani. Labda ulianza kusoma mstari ule ule kwenye kitabu chako tena na tena kwa sababu uliyumbishwa kwa msukosuko.
Lakini huenda nahodha alitoa tangazo: “Tumekumbwa na msukosuko fulani, kwa hiyo tutarekebisha mwinuko wetu na kujaribu kutafuta hewa laini zaidi.” Kwa hilo tangazo, sasa, tatizo lako halikutoweka. Msukosuko ulikuwa bado upo. Lakini pengine ulivuta pumzi na kushusha pumzi nyingi, ukatulia, ukarudia kusoma, na kwa ujumla ulijisikia una amani zaidi kwa sababu uliacha kuangazia msukosuko na badala yake ukazingatia tangazo la rubani.
Unapohamisha mwelekeo wako kutoka kwa kile unachoogopa na kuelekeza kwa Mungu—yule anaye endesha maisha yetu kwa uhakika—utahisi hofu yako ikipungua.
Bwana mwenye neema, ninapoogopa, nataka kuweka tumaini langu kwako. Je! Utanijalia yote ninayohitaji tafadhali — mawazo, kweli, na kutia moyo — ili kwa kweli nipate kufanya hivyo? Wewe si Mungu wa michafuko, bali ni Mungu wa amani. Wakati sijisikii nina amani, nimejitenga na uwepo Wako. Niwezeshe ili niweze kukaa ndani yako. Maneno yako yatakaa ndani yangu, na nipate uzoefu kamili ya amani yako. Katika jina la Kristo. Amina.
Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.
Kuhusu Mpango huu
Unaweza kushinda hisia za hofu. Dkt. Tony Evans anakuongoza kwenye njia ya uhuru katika mpango huu wa usomaji wa kupata ufahamu. Gundua maisha ya furaha na amani ambayo umekuwa ukitaka, unapotumia kanuni zilizowekwa katika mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative