Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ndoa Ya UfalmeMfano

Ndoa Ya Ufalme

SIKU 5 YA 5

Ukitazama maonyesho au filamu zozote za kijeshi, huenda umewahi kusikia jenerali au askari akipiga yowe, "Wanajaribu kutuzunguka!" Katika mbinu za kijeshi, hapa ndipo adui atajaribu kushambulia kutoka upande mmoja au kutoka nyuma. Sababu ya askari kutotaka kuzungukwa ni kwa sababu inawalazimisha kugawanya ulinzi wao.

Shetani anatumia mbinu sawa na hizi dhidi ya ndoa yako. Acha niseme hili kwa njia hii, anatafuta kugawanya na kushinda. Anajua kwamba wakati wanandoa hawana umoja, anaweza kuwaondoa kwa urahisi zaidi. Hata hivyo, iwapo wanandoa wanafanya kazi katika umoja wa kibiblia, wanaweza kusimama imara dhidi ya Shetani na kumshinda

Lakini umoja ni nini? Kwa bahati mbaya, watu wengi wanafikiri kwamba umoja ina maana ya "kufanana." Hii si kweli. Umoja sio usawa – haimaanishi kuwa kama mwenzi wako. Badala yake, umoja unaweza kufafanuliwa kama kundi lolote la watu ambao wana sifa ya kusudi la pamoja, maono au mwelekeo. Umoja haina maana wala haina uhusiano wowote na kufanana, bali yahusu kusonga mbele kuelekea lengo moja. Fikiria kuhusu timu ya mpira wa vikapu. Kuna nafasi tano tofauti kwenye uwanja. Kila nafasi ina sifa ya ujuzi tofauti, utendaji na majukumu. Lakini wachezaji wote watano wanapiga kuelekea kikapu kimoja kwa sababu lengo lao ni sawa.

Mungu hatuitii kupoteza upekee wetu kama mtu binafsi tunapofunga ndoa. Hata hivyo, ndoa yenye afya ni pale uwepo na kazi ya Roho wa Mungu inapita tofauti zetu binafsi. Huu ni umoja, na umoja unaojengwa kutokana na ushirikiano wa kusudi ya pamoja ili kumshinda adui wa pamoja—shetani. Kanuni hii lazima ieleweke, ikubalike na kutafutwa kila mara ikiwa ndoa itakuwa na uzoefu wa ushindi wa kweli.

Usimruhusu Shetani awagawanye. Jikusanyeni kwenye pande zote ya Neno la Mungu, na kupitia sala, undeni msimamo wenye umoja dhidi ya mashambulizi ya Shetani juu ya ndoa yenu.

Je! NI malengo gani ya kiroho ambayo wewe na mwenzi wako mnaweza kuunganikia? kiroho?

Tunatumahi kuwa mpango huu ulikuhimiza. Kwa habari zaidi kuhusu wizara, bofya hapa.

siku 4

Kuhusu Mpango huu

Ndoa Ya Ufalme

Ndoa huja na furaha nyingi na changamoto kubwa. Sababu mojawapo ya changamoto hizo ni kwa sababu tumesahau kusudi la kibiblia la ndoa. Tumemuondoa Mungu na kufafanua ndoa kwa msingi ya furaha. Lakini ndoa ipo ili kumtukuza Mungu kwa kupanua wigo Wake ulimwenguni kote. Katika mpango huu wa siku tano wa kusoma, Dkt. Tony Evans anakupeleka kwenye safari ya ndoa ya ufalme.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/