Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Gundua Kusudi LakoMfano

Gundua Kusudi Lako

SIKU 4 YA 5

Kwenye baadhi ya mashati yangu, herufi zangu za kwanza za jina langu zimeshonwa kwenye pingu – A.T. E. Hakutawahi kuwepo na swali kamwe kuhusu mashati kwamba ni ya nani kwa sababu herufi za kwanza za jina langu zinaonyesha kuwa ni mashati yangu. Ninafanya hivi kwenye mashati ambayo binafsi nimeyatengenezea.

Sasa nina mashati mengine kadhaa ambayo yalinunuliwa kwenye duka. Watu wengi wanaweza kudai kwamba wao pia wana mashati kama yangu, na watakuwa sahihi. Lakini hawangeweza kudai hivyo kuhusu mashati ambayo yana herufi za kwanza ya jina langu zilizoshonwa, kwa sababu mashati hayo yalitengenezwa maalum.

Kitu kinapotengenezwa maalum inamaanisha kuwa kinafaa kwa upekee wako. Imeundwa kwa kukuzingatia wewe. Hiyo ina maana si kwa kila mtu mwingine yeyote kuvaa.

Sisi sote ni wa kipekee. Sisi sote tumeundwa kimaalumu. Hakuna sababu ya kujaribu kuwa mtu mwingine au kuishi maisha ya mtu mwingine. Kwa nini ujitulize kwa hayo ya kawaida wakati kuna kitambulisho na hatima iliyoundwa maalum kwa ajili yako? Kuishi kulingana na hatima yako sio maisha ambayo unajipima wewe huku ukijilinganisha na mtu mwingine. Wala sio maisha ambayo unapima ulichofanya ukilinganisha na kile ambacho mtu mwingine amefanya. Maisha ya hatima ni pale unapopima ulichofanya ukilinganisha na ulichoumbwa kufanya.

Bado watu wengi sana hutumia muda mwingi wa maisha yao kujaribu kuwa mtu mwingine. Kwa nini ujaribu kuwa mtu mwingine, ni swali ambalo ninauliza kila wakati. Mungu tayari ana mmoja wao. Kuna mmoja tu - na wewe ndiye. Mojawapo ya hatua za kwanza za kuishi kulingana na hatima yako inakuja kwa kutambua kuwa ni hatima YAKO. Mungu alikuumba wa kipekee kwa makusudi kwa sababu ana mpango ambao utu wako, asili yako, tabia yako, mawazo, ujuzi na mengine yote yanaweza ndio tu yaweza kutimiza. Jikumbatie - acha kulinganisha. Sitisha mashindano. Acha wivu, kijicho au majuto. Uwe wewe kama alivyokuumba Mungu nawe utakuwa katika njia yako ya kudhihirisha ndani yako kusudi ambalo Mungu amekuumba utimize.

Sala:

Bwana, nisaidie kukumbatia upekee wangu. Nifunulie jinsi sifa hizi maalum ambazo mimi pekee ninazo zinaweza kutumiwa na wewe kwa njia kuu unaponiwezesha kuishi na kutumiza hatima yangu. Nirekebishe ninapokosoa tofauti zangu badala ya kukushukuru kwa ajili yazo.

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Gundua Kusudi Lako

Katika mpango huu wa kusoma kwa ufahamu, mchungaji na mwandishi mashuhuri Tony Evans anakupitisha katika mchakato wa kugundua kusudi lako.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/