Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

TumainiMfano

Tumaini

SIKU 1 YA 3

Kutokuwa na tumaini mara nyingi huja maishani mwako unapojihisi kuwa umefika mwisho, umegonga mwamba. Lakini ningelipenda kutaja hivi, mara kwa mara Mungu huturuhusu tugonge chini kwenye mwamba, kusudi tugundue kuwa Yeye ndiye Mwamba ulioko chini. Kutokuwa na tumaini mara nyingi huzaliwa na ugumu wa maisha, kushindwa na kushushwa moyo. Japo mambo haya yote ni machungu, kuna misimu ambayo Bwana hutumia mateso yetu kutukuza na kututia nguvu. Nyakati hizi ndizo Yeye huona vyema kuondoa kujiridhisha kwetu.

Rafiki, hatupaswi kukimbia matatizo au kujaribu kukabiliana nayo kwa njia itakayotutoa kwenye masomo tunayojifunza. Siyo yenye kupendeza na si yenye furaha, naelewa hilo. Lakini itazalisha ndani yako maisha bora kuliko ulivyodhania, ikiwa utairuhusu na wala usipinge kukua huko. Yesu alisema, “Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.” (Mathayo 5:3). Wale waliovunjika kiroho watabarikiwa kwa sababu watamwona Mungu kwa njia isiyo kama ya wengine. Watakuwa na uzoefu wa uhalisia wake na uwepo wake ukitiririka maishani mwao kwa njia ya kibinafsi na ya kipekee.

Maandiko yanaahidi kwamba Mungu hukaa karibu na wale waliovunjika na huwafanya wenye nguvu kuliko hapo awali. Zaburi 34:18 yasema, “Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa.” Isaya 61:3 inafundisha kwamba, Mungu huwapa waombolezao na waliovunjika, “taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.”

Sote tumeona samani au fanicha ziliyorejeshwa. Urejesho wa samani hujumuisha kuondoa rangi ya kale ukitumia kemikali yenye nguvu. Hiyo huonyesha mianya, nyufa na madoa ya asili ya samani hiyo. Kisha msasa hufanywa mahali ambapo mbao husuguliwa kwa msasa usio laini kusudi ni kuondoa kasoro zilizoko. Baada ya hapo ile samani inakuwa tayari kupokea rangi mpya – ni tayari kwa mwonekano mpya.

Utukufu mpya unaweza kutolewa kwa samani za zamani. Na Mungu anaweza kufanya jambo lilo hilo na wewe.Anaweza kuweka utukufu mpya ndani ya maisha yako ya kale, lakini ni lazima aondoe mawaa yote huku akipiga msasa ngome zilizoko ili kukufikisha mahali pa usafi na utegemezi kwake.

Bwana anatamani kukubariki na kukurejesha, lakini anataka kukubadilisha katika mchakato huo. Wakati mwingine, njia kuu ya uponyaji inahusisha kukumbatia maumivu huku ukielewa kwamba Mungu anakutakia makuu yaliyo mema. Kama vile mwanariadha anayepata maumivu ya kumpeleka kwenye kiwango cha juu zaidi cha uwezo, Mungu mara kwa mara hutumia nyakati za maumivu maishani mwetu kutufanya tuwe wenye nguvu zaidi. Leo nataka umshukuru kwa kile anachofanya na anaweza kufanya kupitia majaribu yanayokukabili. Siulizi umshukuru kwa ajili ya majaribu, kwani hilo huenda likawa ngumu sana sasa hivi, lakini ningependa umshukuru kwa mema anayozalisha kupitia hayo.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Tumaini

Kutokuwa na tumaini ni tauni inayokabili watu wengi wakati moja au mwingine. Hali hii haijahifadhiwa kwa wachache waliochaguliwa. Hata wengi wa mashujaa wetu wa Biblia wanaoheshimika, waliteseka kutokana na kutokuwa na tumaini katika miida fulani fulani. Tony Evans anashiriki mawazo yake jinsi ya kuwa na tumaini, na kushinda hali hiyo ya kukata tamaa katika mpango huu mfupi wa kusoma.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/