Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wema Wetu Na Utukufu WakeMfano

Wema Wetu Na Utukufu Wake

SIKU 3 YA 3

Mojawapo ya ugumu wetu katika kubaki kwenye njia sahihi tunapoelekea kwenye kusudi letu ni kwamba hatuoni mwisho wake. Tunakerwa na kuhisi kupotea wakati hatuoni tunakoelekea. Je, umewahi hisi kukerwa ulipokuwa ukiendesha gari na ukapotea? Au umewahi kuwa pamoja na mtu aliyepata kukasirika wakati alipokuwa akiendesha gari na akapotea? Lakini wakati ramani, dira ya setilaiti au maelekezo kutoka kwa mtu usiyemfahamu anapokuelekeza njia — kero huondoka. Hii ni kwa sababu mwisho ulionekana.

Kinachotokea kwetu, katika kumfuata Mungu kwenye njia za uongozi wake na uangalizi ni kwamba yeye daima hatupi maelekezo hadi mwisho kabisa. Yeye hatupi mwonekano kamili wa ramani ili tuweze kuona kila kona ambayo hatimaye tutaifanya. Anatupa kuona kidogo tu hapa au mwelekeo huko, lakini mara chache sana hutonyesha picha nzima. Kwa hivyo, mara nyingi watu huishi katika hali ya kudumu ya kuvunjika moyo bila kujua jinsi kila hatua, kila siku, kila mfuatano wa hali au mazungumzo yanatuelekeza mahali palipo pazuri. Bila mtazamo kamili wa riziki inayofungamana na kujisalimisha kwa ukuu wake Mungu, mafadhaiko haya yanaweza kuongezeka na kuwa msururu mkubwa wa hisia zinazokutishia kimihemko kama maporomoko ya theluji katika siku ya kimbunga.

Tunatumahi kuwa mpango huu ulikuhimiza. Kwa habari zaidi kuhusu wizara, bofya hapa.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Wema Wetu Na Utukufu Wake

Katika mpango huu kusoma kwa ufahamu, Mchungaji na mwandishi mashuhuri Tony Evans anaelezea jinsi kila kitu tunachofanya ni kulingana na kusudi kuu la Mungu, na yote hufanya kazi kulingana na mapenzi yake kwa wema wetu na utukufu wake.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/