Kugeuka Kutoka Katika Masuala Ya MihemkoMfano
Mojawapo ya ngome kuu za kimihemko ambayo watu hukumbana nayo leo inajulikana kama utegemezi. Kuna maneno mengine ambayo yanafafanua maana ya ngome hii ihusishayo uhusiano aidi ya mmoja – maneno hayo ni kama vile kuwapendeza watu na uraibu wa mitandao ya kijamii. Lakini, kwa kuanzia, hebu tuangalie utegemezi.
Utegemezi ni njia mojawapo ya kukabiliana (aina moja ya ngome ya kimihemko) inayomwezesha mtu kukabiliana – ingawa kwa njia mbovu – na upungufu anaohisi. Huenda kuna ukosefu wa uthamana wa binafsi, kujistahi au hisia kali sana za kukataliwa. Hata hivyo, utegemezi kwa kawaida ni hali ile ya kumhusisha mtu au watu kurekebisha kilichovunjika. Ninaiita hii kuwa na ngome ya watu.
Mungu ndiye pekee aliye na nguvu na uwezo wa kukidhi mahitaji yetu. Shida huingia mara tunaposisitiza kuwageukia wengine kabla ya kumgeukia. Katika neno lake lote, twasoma jinsi Mungu anavyotumia watu katika maisha ya wengine. Hata hivyo, hatusomi popote ambapo Mungu anapendezwa tunaporuhusu watu na vitu vingine vichukue mahali pake. Kwa kweli, kinyume chake ni kweli; tumeunda sanamu ya mihemko. Hata uraibu wa mitandao ya kijamii yaweza kuwa kwenye kiwango cha ibada kwa sanamu ya mihemko.
Kuna mpaka mwembamba mzuri kati ya kufurahia uhusiano fulani au kufaidika na miunganisho ya mitandao ya kijamii na ugatuzi wa mahusiano ya mihemko au ulinganisho. Watu na mahusiano ni karama tunapaswa kufurahia. Lakini pia, twahitaji kuwa waangalifu tusije tukaruhusu mihemko yetu ikageuka na kuwa ngome ya huzuni, upweke, husuda, shaka au woga.
Wahitaji kujikumbusha kwamba, katika Kristo, una kila kitu unachohitaji. Hauhitaji kushikilia kitu kutoka kwa mtu mwingine ili kukufanya ukamilike.
Je! Ni nini au nani unayetegemea kwa hisia zako za kijithamini?
Tunatumahi kuwa mpango huu ulikuhimiza. Kwa habari zaidi kuhusu wizara, bofya hapa.
Kuhusu Mpango huu
Wakati ambapo maisha yako yanatoka katika upatanisho wa neno la Mungu, hakika ni kwamba, utakabiliwa na hali ngumu yenye matokeo yaletayo uchungu. Mihemko yako inapokosa kudhibitiwa nayo ikaanza kuamua ustawi wako, utajikuta umejifungia katika gereza la kujitengenezea ambalo linaweza kuwa vigumu kwako kutoroka. Wahitaji usawaziko, na kujifunza jinsi ya kumtumaini Mungu. Mruhusu Tony Evans akuonyeshe njia ya uhuru wa kimihemko.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/