Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuongea na Mungu kwa MaombiMfano

Talking With God In Prayer

SIKU 1 YA 4

MUNGU ANAHAMU NA WEWE

KUONGEA NA MUNGU
Mshukuru Mungu kwa mapenzi yake na kukujali. Muulize akuonyeshe ni kiasi gani anataka wewe uongee naye kila siku.

KUPIGA MBIZI NDANI
Panga idadi ya glasi ndogo karibu na sinki jikoni. Moja baada ya nyingine, jaza glasi hizo. Jadilianeni jinsi mnaweza kujaza kila chombo nyumbani na maji bado yatatiririka kutoka kwa bomba Katika njia sawa sawa na hiyo, hamu ya Mungu kwako haina mwisho.

KWENDA CHINI SANA
Mungu anapatikana kwako kila wakati. Kama vile unaweza kujaza glasi nyingine kwa maji kwa kuwasha bomba, ndivyo unaweza kufurahia uwepo wa Mungu kwa kwenda kwake kwa maombi. Soma Isaya 30:18: "Bwana anahamu ya kuwa mwenye neema kwako; anainuka kukuonyesha huruma. Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa haki. Heri wote wanaomgonja!" Mungu anataka umkaribie, ndiposa ujazwe na upendo Wake na amani, kwa sababu anaufahamu ya kile ambacho ni bora kwako. Ingawa Mungu hufanya kazi kwa niaba yetu, Anakutaka umjibu, ukionyesha nia ya kumshirikisha katika maisha yako. Njia moja ya kufanya hayo ni kwa kuongea na Yeye kila siku.

KUZUNGUMZA NA KILA MMOJA
- Ni nani unayependa kuzungumza naye, na ni kitu gani kinamfanya mtu huyu kuwa unayependa kuzungumza naye?
- Nisimulie wakati mmoja ambao ulitaka kwa kweli kuzungumza na huyu mtu. Mbona ulikuwa na hamu sana ya kuzungumza na huyu mtu?
- Ni kwa nini Mungu anahamu ya kuwa mwenye neema kwako?

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Talking With God In Prayer

Maisha ya familia, unaweza kuadimika, na tukakosa kupata wakati wakati wa kuomba - wacha hata kukumbuka kuwasaidia watoto wetu kuendeleza tabia ya kumuhusisha Mungu katika siku zao. Katika mpango huu, familia yako itaona ni kiasi gani Mungu anataka kusikia kutoka kwetu na jinsi maombi yanaimarisha uhusiano wetu na Mungu na baina yetu. Kila siku ina kumbusho la maombi, kusoma maandiko na maelezo mafupi, shughuli za kufanya, na maswali ya majadiliano.

More

Tungependa kushukuru Focus on the Family kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.FocusontheFamily.com