Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Mfano
Wajibu wa kikristo ni kuishi kama Neno la Mungu linavyoelekeza. Hiyo ndiyo ishara ya wokovu na utetezi wa kweli wa imani. Wasio Wakristo hutusumbua kwa sababu ya mwenendo huo ili tuache tukiaminicho. Tusikate tamaa kwani tumepewa kuteseka kama fungu la wito wetu sawia na tulivyopewa wokovu. Mateso hutuimarisha. Hivi ndivyo Paulo anavyokiri akisema,Na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi(Rum 5:3-5). Maadui wakiona tumesimama imara, watalazimika kukubali tumeokolewa. Kwa hiyo Wakristo hawapaswi kuogopa uadui bali watunze mienendo yao na kutetea imani.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/