Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumeMfano

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

SIKU 18 YA 20

Paulo anapofika Kaisaria, anashtakiwa mbele ya gavana, Felix. Paulo anajitetea, akishuhudia kuwa tumaini lake ni Mungu wa Israeli na anashiriki tumaini sawa la kufufuka na washitaki wake. Felix haoni sababu ya kumshutumu Paulo, lakini hajui cha kumfanyia pia, kwa hivyo anamtia kuzuizini bila sababu ya kisheria kwa miaka miwili. Wakati wote Paulo akiwa kizuizini, mke wa Felix anaomba kusikia kutoka kwa Paulo na Yesu. Felix anasikia pia na anaogopeshwa na matokeo ya Ufalme wa Yesu. Anaepuka mjadala huo lakini bado anamuita Paulo mara kwa mara akiwa na matumaini ya kupokea rushwa kutoka kwake. Hatimaye nafasi ya Felix inachukuliwa na Porkio Festo, na kesi ya Paulo inachunguzwa tena mbele ya Wayahudi ambao bado wanataka afe. Paulo anakana makosa tena, na kwa kujibu, Festo anamuuliza Paulo ikiwa yuko tayari kuhamisha kesi hadi Yerusalemu. Lakini Paulo hakubali na anakata rufaa ili kushitakiwa huko Rumi mbele ya Kaisari. Festo anaidhinisha ombi lake. Sasa kama Yesu alivyosema tu (Matendo ya Mitume 23:11), Paulo atatekeleza kusudi la Yesu ndani ya Rumi.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

• Pitia kujitetea kwa Paulo mbele ya Felix (tazama 24:10-21) na Festo (tazama 25:8-11). Unatambua nini? Ni maneno au virai vipi vinakuvutia zaidi?

• Paulo alizungumza kuhusu uadilifu, kujidhibiti, na hukumu inayokuja (24:25). Baadhi ya wasikilizaji wa Paulo wanatiwa hofu na kumgeukia Mungu, lakini wengine wanaogopa na kujaribu kuepuka hata kuliongelea hilo. Jibu lako ni lipi?

• Badilisha tafakari yako kuwa ombi kutoka moyoni mwako. Ongea na Mungu kuhusu hofu yako, na muombe ujasiri wa kujifunza na kutekeleza ujumbe wa Yesu.

siku 17siku 19

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com