BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - LukaMfano
Tunapoelekea kwenye sura zinazofuata za kitabu cha Luka, hebu tukumbuke maneno ya Yesu baada ya kusoma maandiko ya Isaya. Yesu ndiye aliyekuwa akirejelewa na Isaya tangu mwanzo. Yeye ndiye mtiwa mafuta atakayeleta habari njema kwa maskini, atakayewaponya waliovunjika moyo na kuwakomboa mateka.
“Leo maandiko haya yametimia,” Yesu alisema. Simulizi zinazofuata tamko hili zinaonyesha matendo yanayohusiana na habari njema za Yesu. Katika sehemu hii ya kitabu cha Luka, habari njema inaonekana pale Yesu anapowawezesha wavuvi waliochoka kupata samaki, kumponya mtu mwenye ukoma, kumsamehe mtu aliyepooza na kumuajiri mtoza ushuru aliyedharauliwa na jamii awe sehemu ya huduma yake. Yote haya yanasababisha uhasama kati yake na vikundi vya kidini, na zaidi ya hayo, Yesu anamponya mtu mwenye mkono uliopooza siku ya Sabato, siku ya kupumzika. Viongozi wa dini wanaghadhabishwa. Hawaelewi kwa nini Yesu anavunja sheria zao za Kiyahudi za Sabato na anajumuika na watu wanaondeshea maisha yao kwa kufanya maamuzi mabaya.
Lakini Yesu anawatetea wanyonge na anawafafanulia viongozi wa kidini kiini cha sheria ya Kiyahudi na anawaeleza kuhusu Ufalme wake unaenda kinyume na matarajio ulivyo wa kipekee. Anawaeleza kuwa yeye ni kama daktari anayewashughulikia walio wagonjwa sio wenye afya. Anaweka wazi kuwa siku ya sabato inahusu urejesho kwa wanaoumia. Yesu ndiye anayerejesha. Hawachagui walio wakuu kwenye jamii; badala yake, anarejesha hadhi ya wanaoteseka. Na wanaoteseka wanapomfuata, wanapata urejesho na wanajiunga naye kwenye kazi yake.
Soma, Tafakari, kisha Ujibu:
•Wanaopokea uhuru wa urejesho wa Masihi (Isaya 61:1-3) ndio wanaoshiriki uhuru wao wa urejesho kwa wengine (Isaya 61:4). Je, Yesu anatimiza vipi unabii wa Isaya kwenye kitabu cha Luka?
•Je, umeshuhudia vipi uhuru wa urejesho wa Yesu? Je, unaweza kushiriki uhuru huo kwa njia ipi wiki hii?
•Je, Simoni, Yakobo, Yohana, umati, mwenye ukoma, aliyepooza pamoja na marafiki zake, Mafarisayo na walimu wa torati walipokea vipi habari njema za Yesu? Je, unampokea vipi leo?
•Kusoma na kutafakari kwako kukuchochee kuomba. Mshukuru Mungu kwa ajili ya moyo wake wa kurejesha. Nena naye kuhusu hali unayohisi inahitaji urejesho katika maisha yako mwenyewe na kwenye jamii. Anasikiliza.
Kuhusu Mpango huu
Shirika la BibleProject liliandaa mwongozo wa Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio Sehemu ya 1 kuwahimiza watu binafsi, vikundi vidogo na familia kusoma kitabu chote cha Luka kwa siku 20. Mwongozo huu unajumuisha video za katuni, muhtasari wa uchambuzi na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia wahusika kumfahamu Yesu na kufuatilia mtiririko wa mawazo ya Luka pamoja na kuyaelewa mafunzo yake.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com