Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - LukaMfano

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

SIKU 14 YA 20

Kwenye sehemu hii inayofuata ya kitabu cha Luka, Yesu anawaponya vipofu na anazidi kutoa mafundisho ya kiroho kuhusu maana ya kuishi katika Ufalme wa Mungu unaoenda kinyume na matarajio. Lakini kabla ya mtu yeyote kuanza kuishi maisha ya Ufalme wa Mungu kupitia maombi na kuonyesha ukarimu kwa maskini, sharti kwanza aingie. Hakuna anayeweza kuingia kwenye Ufalme wa Mungu isipokuwa kwanza anyenyekee na amtegemee Mungu kwa mambo yote. Wengine wanajitegemea wao binafsi na hawaelewi hili, hivyo anatoa mfano huu. Alisimulia kama ifuatavyo.

Siku moja, watu wawili wanakwenda hekaluni kuomba. Mmoja ni Mfarisayo, anayetambulika kwa ujuzi wake wa Maandiko na uongozi wake hekaluni, na wa pili ni mtoza ushuru, anayedharauliwa kuwa kibaraka mfisadi anayefanya kazi na Warumi. Mfarisayo anaomba akisema jinsi alivyo mtakatifu zaidi kuliko watu wengine wote. Anamshukuru Mungu kwa hili. Lakini yule wa pili, mtoza ushuru, hata hawezi kutazama juu anapoomba. Anapiga kifua chake kwa huzuni na kusema, “Ee Mungu, nihurumie, mimi ni mwenye dhambi!” Yesu anamalizia simulizi yake kwa kusema kuwa mtoza ushuru ndiye pekee aliyekwenda nyumbani akiwa mkamilifu mbele za Mungu. Anafafanua jinsi mageuzi haya ya kihadhi na wadhifa yanayostaajabisha yanavyofanya kazi katika Ufalme wake: “Kila anayejiinua atashushwa, lakini anayenyenyekea atainuliwa.”

Luka anasisitiza mada hii ya unyenyekevu kwa kuzingatia mafundisho ya Yesu na tukio lingine katika maisha ya Yesu. Luka anafafanua kuwa kuna wakati kina mama na baba waliwaleta watoto wao wadogo kwa Yesu ili awabariki. Wanafunzi wanaona kuwa huu ni usumbufu. Wanawakemea na wanajaribu kuwafukuza. Lakini Yesu anawatetea watoto kwa kusema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie, maana Ufalme wa Mungu ni wao.” Anamalizia kwa kutoa onyo na mwaliko huu, “Mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauona kamwe.”

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

•Soma simulizi inayosimuliwa na Yesu katika Luka 18:10-14. Unatambua nini? Je, unawezaje kujifananisha na Mfarisayo na mtoza ushuru? Je, kuna hatari zipi za kuwa mwenye kiburi na mwenye kujilinganisha? Kama yule Mfarisayo, sisi pia tunaweza kujaribu kujihesabia haki mbele za Mungu kutokana na matendo yetu, lakini inamaanisha nini kumruhusu Mungu kutuhesabia haki kwa rehema zake?

•Fikiria jinsi watoto wana utegemezi. Je, unawezaje kufafanua maana ya kuwa kama mtoto? Linganisha utegemezi wa watoto na ufafanuzi wa Luka kuhusu mioyo yenye kiburi ya waliosikiliza simulizi iliyosimuliwa na Yesu (soma Luka 18:9). Unatambua nini?

•Kusoma na kutafakari kwako kukuchochee kuomba. Mshukuru Mungu kwa rehema zake, mtegemee yeye pekee na umwombe akupe uwezo wa kuwa mwenye rehema kwa wengine kama anavyokuhurumia.

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 1 - Luka

Shirika la BibleProject liliandaa mwongozo wa Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio Sehemu ya 1 kuwahimiza watu binafsi, vikundi vidogo na familia kusoma kitabu chote cha Luka kwa siku 20. Mwongozo huu unajumuisha video za katuni, muhtasari wa uchambuzi na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia wahusika kumfahamu Yesu na kufuatilia mtiririko wa mawazo ya Luka pamoja na kuyaelewa mafunzo yake.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com