Biblia i HaiMfano
Biblia Hubadilisha Kilakitu
Fikiria kila kitu ni giza na pasipo na umbo mpaka Mungu alipopulizia pumzi ya neno lake, " na iwe nuru." Ghafla, kila kitu hubadilika. Nuru ikalichoma giza, na kitu ambacho kilikuwa kinaonekana hakiwezekani sasa kinaonekana waziwazi.
Mungu yuleyule aliyeziumba mbingu kwa neno moja anaendelea kupulizia uzima mpya ulimwenguni kupitia nguvu ya neno lake. Neno la Mungu linaendelea kulichoma giza. Neno la Mungu hubadili maisha na hurejeza mioyo inayoumia. Neno la Mungu li hai na linatenda kazi kwa sababu Yu hai na anatenda. Na tunauwezo wa kulifikia neno lake.
Kwa kadri tunavyojifunza Biblia, ndivyo tunavyogundua kwamba Mungu anataka kila mmoja ulimwenguni apate kurejea kwake kimuhusiano, kutenda binafsi.
Haijalishi ni mateso na majaribu kiasi gani tunapitia, neno la Mungu litaendelea kutoka na kuchoma giza. Neno lake litaendelea kubadili watu kama Ghana, Diya, watu wa Popoluka, Samuel Ajayi Crowther, na William Tyndale. Na maneno yake yana nguvu ya kukubadilisha.
Kwa hiyo tulia na utafakari kuhusu hadithi yako. Neno la Mungu limekubadilisha namna gani? Na kwa njia zipi Mungu anaweza kukuletea maandiko hai maishani mwako sasa hivi?
Shangilia kile ambacho Mungu amekifanya maishani mwako mpaka sasa, na angalia anachofanya kwa ulimwengu unaokuzunguka.
Kwenda mbele, changua kuwa sehemu ya hadithi Mungu anayosimulia. Ni hadithi iliyoanza aliposema na ulimwengu ukawa, na itaendelea mpaka Yesu atakaporudi--hadithi inayopita historia na inaendelea kuubadili ulimwengu.
Kuhusu Mpango huu
Tangu mwanzo wa wakati, neno la Mungu kwa uhakika limerejeza mioyo na mawazo ya watu--na Mungu hajamaliza bado. Katika mpango huu wa siku 7, hebu tusherehekee nguvu ya maandiko inayobadirisha kwa kuangalia kwa makini jinsi Mungu anavyotumia Biblia kubadili historia na maisha duniani kote.
More