Soma Biblia Kila Siku Machi 2021Mfano
Huko Korintho utume na wito wa Paulo ulitiliwa mashaka. Hapa mtume anashuhudia juu ya wito na sifa zake za kitume. Amekutana uso kwa uso na Kristo mfufuka: Ikawa[Paulo] anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe(kama una nafasi, tafuta kusoma habari zote za Mdo 9:1-18). Maisha yake yalibadilika kutoka kulitesa kanisa hadi kuitangaza Injili. Sasa Mungu anamtumia kwa kazi yake. Ni ushahidi mwingine kwamba ameitwa na Kristo mwenyewe. Hata Paulo aliacha kudai iliyokuwa haki yake ili asiiwekee kizuizi chochote Habari Njema ya Kristo: Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo(m.12). Je, wewe u tayari kufanya vivyo hivyo?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz