Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

SIKU 5 YA 31

Waalimu wa uongo hujifanya wanamwakilisha Yesu Kristo, kumbe wanajiwakilisha wenyewe na mambo yao. Tumia maswali yafuatayo katika kuainisha ufuasi wa kweli na wa uongo: Je, fundisho hili linathibitisha Maandiko Matakatifu? Je, mfundishaji anamthibitisha Yesu Kristo kuwa ni Mwokozi? (Zingatia 1 Yoh 4:1-3, Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani). Maisha ya mfundishaji, mhubiri n.k., je, yanafuatana na maadili ya kibiblia? (Zingatia Mt 12:33-37, Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana.Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa).

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz