Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano
Mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi(m.11). Kunahitajika kazi ngumu na nzito inayoambatana na kujitoa muhanga katika kuyatatua matatizo yanayolikabili kanisa la sasa. Matatizo haya ni pamoja na mafarakano, ukabila, ubinafsi, ubadhirifu wa mali za umma na kanisa n.k. Haya yasipoondolewa yanazuia kuenea Injili kwa haraka. Pia katika nyaraka zake nyingine, Paulo anawatakia Wakristo amani (soma k.m. Rum 15:33 na Efe 6:23). Basi, lengo la kanisa liwe ni kutafuta amani. Ombea juu ya umoja na amani ya Kristo ili vitawale kanisa na taifa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz