Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano
Kuanzia katika mahusiano ya mtu na mtu, familia, majirani, kazini, vyama vya kisiasa, nchi na nchi, kabila na kabila, tunashuhudia mafarakano. Siku za leo haya mafarakano yako hata ndani ya kanisa letu. Shabaha ya Kristo ni kuleta amani. Hiyo anafanya kwa njia ya upatanisho. Kristo Yesu ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga.Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani.Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba.Akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa karibu.Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja(Efe 2:14-18). Ukishapatanishwa na Mungu, kwa kusamehewa dhambi, hatua inayofuata ni wewe kuwa mjumbe wa upatanisho kuanzia pale ulipo. Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu(2 Kor 5:20).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz