Kusikia kutoka Mbinguni: kusikiza Mungu kila siku.Mfano
“Ongea, Bwana, Mtumishi Wako Anasikiza”
Mungu daima, uongea na watu wake wazi wazi. Kupitia kwa makuhani na manabii, alithihirisha kweli ambayo ilitoa uhai kwa wale wanaompenda na kumtegemea. Na anapenda kuongea na watu wake! Lakini kama hatuwezi kuona na kusikia, maisha yetu kama wafuasi wa Kristo yatakuwa magumu.
Unaweza fikiria neno la mungu likiwa nadra? Kukaa masiku, labda hata mika, bila kusikia kutoka kwa mungu. Inatishia na kuleta kukosa tumaini. Lakini hilo ndilo lililofanyika katika Samweli wa kwanza. Wakati watu wa mungu walipokuwa wanangojea sauti ya mungu, mungu aliamua kujithihirisha kwa kijana mdogo.
Kijana Samweli bado hakuijua sauti ya mungu. Kwa hivyo aliposikia wito, aliitika vile alivyojua kuitika. Alimkimbilia binadamu! Lakini kupitia kwa hekima ya Eli, Samweli alianza kuelewa sauti ilikuwa ni ya nani.
Sauti Ya Mungu Yaweza Kujulikana. Tunahitaji Tu Kujua Ni Nini Cha Kusikiliza!
Nilisoma hii hadithi nikiwa kijana mdogo katika semina ya Compassion International ambayo nilihudhuria, na ilinihamasisha sana. Nikiwa naishi katika umaskini uliokithiri, nilitamani sana Mungu ajithihirishe kwangu kwa njia kuu na ya uwazi kama hii. Lakini ningefanya nini kama kweli mungu angejithihirisha kwangu? Je angetaka nifanye nini ni maisha yangu?
Jifunze kusikiza sauti ya kweli badala ya shaka na kukata tamaa. Funza sikio lako kusikia habari njema ya Mungu! Bwana alitupa neno lake kwa njia ya kitabu- kwa hivyo soma ukweli ambao uko kwa biblia kwa ajili yako. Tafuta mshauri anayeijua sauti ya mungu na msome biblia pamoja naye. Jiunge na kundi la waumini wanahomjua na kumpenda bwana, na ambao wanaweza kukusaidia katika kuelewa sauti ya mungu.
Eli alimfunza samweli jinsi ya kujibu sauti ya bwana: “ongea, bwana, mtumishi wako anasikiza” Tunapaswa kumjibu mungu kama Samweli kila mara mungu anatuzungumzia.
Bwana anataka kujithihirisha kwa watu wake. Anataka atuongoze. Je waijua sauti ya mungu? Je unatafuta mwongozo kuhusu hatua zijazo za maisha yako, biashara, elimu, jamii ama huduma? Kama hili ndilo ombi lako, basi omba nami sasa, “ nena, bwana, mtumishi wako anasikiza”
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Bwana yu hai na ni mkamilifu leo, na uongea na kila mtoto wake moja kwa moja. Lakini wakati mwingine, inaweza kuwa ngumu kumuona na kumsikia Mungu. Kupitia kuchunguza hadithi ya safari ya mtu mmoja ya kufahamu sauti ya Mungu katika mabanda ya Nairobi, utasoma vile ilivyo kumsikia na kumfuata Mungu.
More
Tunapenda kushukuru Huruma ya Kimataifa kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.compassion.com/youversion