INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TANOMfano
YESU AMFUFUA MWANA WA MJANE
"11-12 Baadaye kidogo, Yesu alikwenda katika mji mmoja ulioitwa Naini. Nao wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu walikwenda pamoja naye.Alipokaribia lango la mji, alikutana na watu waliokuwa wamebeba maiti wakitoka nje ya mji. Huyu aliyekufa alikuwa mwana pekee wa mwanamke mjane. Umati mkubwa wa watu wa mji ule ulikuwa pamoja na huyo mwanamke."
13 Bwana Yesu alipomwona yule mjane, moyo wake ulimhurumia, akamwambia, “Usilie.”
14 Kisha akasogea mbele akaligusa lile jeneza na wale waliokuwa wamelibeba wakasimama kimya. Akasema,
“Kijana, nakuambia inuka.”
15 Yule aliyekuwa amekufa akaketi akaanza kuongea, naye Yesu akamkabidhi kwa mama yake.
16 Watu wote wakajawa na hofu ya Mungu, nao wakamtukuza Mungu wakisema,
“Nabii mkuu ametokea miongoni mwetu, Mungu amekuja kuwakomboa watu wake.”
17 Habari hizi za mambo aliyofanya Yesu zikaenea Uyahudi wote na sehemu zote za jirani.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kushukuru GNPI-AFRIKA kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://gnpi-africa.org/