Bila UtulivuMfano
Jana, tuliona jawabu wa mahangaiko yetu linaweza kupatikana kwenye mapumziko ya mfano wa sabato kutoka vyanzo vya mahangaiko. Kesho, tutaangalia ni jinsi gani sisi kama wakristo tunafanya katika karne hii ya 21. Lakini kwanza, lazima tuangalie ni kivipi sabato siyo kwa wakristo wa leo. Na mahali pa kuanzia ni chanzo cha sabato yenyewe.
Wakati Mungu alipozitoa Amri Kumi kwa Musa katika mlima Sinai, aliagiza wana wa Israeli kupumzika siku ya saba ya juma. Hii ilikusudiwa kuwa ishara ya agano na Mungu na watu wake. Na, ni wazi, sabato ilitengenezwa baada ya siku ya Mungu mwenyewe kupumzika kutokana na kazi ya uumbaji siku ya saba.
Katika Agano la Kale, sabato ilifuatwa kwa sheria na taratibu kali. Kwa mfano, wana wa Israeli walikatazwa kuwasha moto ( Kutoka 35:3), kukusanya chakula ( Kutoka 16:23-29), na kuuza vitu sokoni ( Nehemia 10:31). Na adhabu yake kwa kukiuka kwa makusudi sabato ilikuwa si kitu kingine zaidi ya kifo ( Kutoka 31:14-15).
Kwa muda, wana wa Israeli waliichukulia sabato kwenye sheria zaidi, kiasi kwamba, Yesu alipokuja duniani, waliona hata kuponya wagonjwa siku ya sabato ni dhambi. Mafarisayo walipomuona Yesu akiponya na kukusanya mbegu shambani siku ya sabato katika Mathayo 12, walimkabili, wakionyesha kwamba hakutii sheria. Yesu aliwajibu kwa kutangaza "kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato" ( Mathayo 12:8) akionyesha kwamba agano jipya limekuja katika Kristo. Katika tukio hilohilo kwenye kitabu cha Marko, Yesu alinukuliwa akisema " sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sababo" ( Marko 2:27). Kwa maneno mengine, Yesu anasema kupitia kwake, sabato simagizo la kisheria. Badala yake, ni zawadi ya neema kwa wenye mahangaiko.
Yesu alimaanisha nini aliposema sabato ni kwa wanadamu? Ni jinsi gani yawezekana kuchukua zawadi hii kimatendo? Na tunawezaje kupumzika mara kwa mara leo, pasipokufanya mapumziko yetu sheria na kudhoofisha maisha yetu? Hayo ni maswali tutakayojibu siku ya mwisho ya mpango huu
Kuhusu Mpango huu
"Mioyo yetu haina utulivu mpaka ipate ulivu kwako." Haijawahi kutokea kuwa wengi wetu tukakosa utulivu Agustine alielezea kwa hii sentesi maarufu. Lakini suluhisho kwa kukosa utulivu wa kweli kwetu ni nini? Huu mpango wa siku tatu utakuonesha, suluhisho kwa sehemu katika kuona vitendo vya kale vya sabato kwa lenzi tofauti ya "wewe" -- Yesu ndie mwanzo wa amani.
More