Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Injili Ulimwenguni - Sehemu 4Mfano

Injili Ulimwenguni - Sehemu 4

SIKU 5 YA 7

Sifa za heri  

Mathayo, Tomasi. Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni aliyeitwa Zelote,Yuda mwana wa Yakobo na Yuda Iskariote, ambaye ndiye aliyemsaliti Yesu.

“Heri walio maskini wa roho,maana hao Ufalme wa Mbinguni ni wao.” 

Heri wale wanaohuzunika,maana hao watafarijiwa.

Heri walio wapole,maana hao watairithi nchi.

Heri wenye njaa na kiu ya haki,maana hao watatoshelezwa.

Heri wenye huruma, maana hao watapata rehema.

Heri walio na moyo safi,maana hao watamwona Mungu.

Heri walio wapatanishi,maana hao wataitwa wana wa Mungu.

Heri wanaoteswa kwa sababu ya haki, maana hao Ufalme wa Mbinguni ni wao."

Heri ninyi watu watakapowashutumu na kuwatesa na kunena dhidi yenu mabaya ya aina zote kwa uongo kwa ajili yangu.

Furahini na kushangilia kwa maana thawabu yenu ni kuu.

Andiko

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Injili Ulimwenguni - Sehemu 4

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana.

More

Tungependa kumshukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org/