Somabiblia Kila Siku 3Mfano
Shetani alimwingia Yuda (m.27). Lakini kuanguka kwake hakukuanza siku hiyo. Kuanzia huko nyuma alitunza mfuko wao. Lakini alianza kuiba fedha hizo (m.29; ling. Yn 12:4-6: Yuda Iskariote ... akasema, Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa dinari mia tatu, wakapewa maskini? Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwivi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo). Upendo wake kwa Yesu ukapoa. Mwisho akaamua kuwasaidia Wayahudi kumkamata Yesu ili kupata fedha nyingi. Hilo ni onyo kwetu! Mara tukiona dhambi yoyote ikitaka kuingia katika mawazo yetu tukiri mbele ya Yesu! Maana dhambi ikishapata nafasi huzidi kupata nguvu na mwisho hutuangusha! Kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike (Yak 1:14-16).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
SomaBiblia Kila Siku 3 ni mpango mzuri wa kukusaidia kusoma Biblia kwa njia rahisi. Ufafanuzi wa somo la kila siku unakupa mwanga na kiu ya kuendelea kulitafakari Neno la Mungu ukiwa peke yako au pamoja na wenzako.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz