Kupata Uhuru kutokana na KufadhaikaMfano
Usiruhusu kufadhaika kuyaendesha maisha yako.
Kufadhaika ni changamoto kwetu sisi sote. Lakini haipaswi kuwa hivyo. Mara nyingi, tunaona kufadhaika kama jambo ambalo lazima tulikabili, lakini Yesu kwa kweli anataka tuwe na uhurukutokakufadhaika kupitia amani Yake.
Sasa, ebu tuyapate mambo kwa usawa. Hakuna njia ya urahisi ya kuondoa mfadhaiko milele. Kufadhaika ni hisia, ama jibu lenye taharuki kwa jambo ambalo akili yako inaona lina hatari. Na hili linaweza kama kweli kuwa jambo zuri, kwa sababu hisia hii inakuepusha hatari, kukuweka motisha ufanye uamuzi wenye busara, ama inakusaidia kufanya mabadiliko yanayo stahili. Lakini wakati kufadhaika kunaanza kuchukua uskani katika maisha yetu- hapo ndipo tunakua katika shida.
Kwa hivyo, labda swali sio ni vipi tutaepuka kufadhaika. Uliza swali bora zaidi: Je tunaweza kubadilisha vile tunavyo tafsiri na kukabiliana na mafadhaiko? Haya ni mambo matatu yanayoweza kukusaidia kuamua dhidi ya kufadhaika.
- Usiruhusu kufadhaika kuyaendesha maisha yako.Ruhusu mfadhaiko usio na madhara kukusaidia unapofanya uamuzi, lakini usiruhu kufadhaika kuweka wingu katika maamuzi yako. Muulize Mungu akupatie uwazi kama kufadhaika kwako kuna kupotezea nafasi ambayo Anakupatia.
- Achilia Udhibiti. Hakuna kinacholisha mafadhaiko kama udhibiti. Yesu anatuitia uhuru kutokana na mizigo mizito. Lakini huu ndio mtego - lazima tuje kwake. Nenda mbele za Mungu na uweke wazi mafadhaiko yako mbele yake Gharama ni udhabiti, lakini zawadi ni uhuru, na pumziko. Uliza hekima.Muulize Mungu kama kuna kitu chochote ambacho kufadhaika kunaweza kukufundisha kuhusu jinsi umekua ukiishi hivi karibuni. Je kuna sehemu katika maisha yako ambayo lazima uache kuiendesha kivyako? Je umejiwekea majukumu kipita kiasi? Muulize Mungu akurekebishe kwa ukarimu, akuongoze na kukuelekeza katika kina cha kufadhaika kwako, kisha umuulize abadilishe kufadhaika kwako na nguvu zake.
Mjadala
- Unawezaje badili mtazamo wako kuhusu kufadhaika?
- Kufadhaika kwako kunakufundisha nini kuhusu jinsi unavyo ishi maisha yako?
- Ni baadhi ya mambo gani unayo hitaji kuyaachilia ili upate amani?
Kuhusu Mpango huu
Kufadhaika huwa, lakini hakufai kuyaendesha maisha yako. Kumpitia Kristo, tunaweza kuibadilisha, kuiona upya na kuitafsiri upya. Kama unapata changamoto na kufadhaika, angalia mpango huu wa Bibilia wa siku 5 ili ujifunze kupata uhuru na amani.
More