Zekaria 4:6-7
Zekaria 4:6-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi. Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie.
Zekaria 4:6-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Naye akaniambia pia niseme neno hili la Mwenyezi-Mungu kumhusu Zerubabeli: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: Huwezi kushinda kwa nguvu au kwa uwezo wako mwenyewe, bali kwa msaada wa roho yangu. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.” Tena, akaongeza kusema: “Je, mlima huu ni kizuizi? La! Wewe Zerubabeli utausawazisha. Wewe utaanzisha ujenzi mpya wa hekalu, na wakati utakapoliweka jiwe la mwisho, watu watashangilia wakisema, ‘Ni zuri! Naam, ni zuri!’”
Zekaria 4:6-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi. Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie.
Zekaria 4:6-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha akaniambia, “Hili ni neno la BWANA kwa Zerubabeli: ‘Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho yangu,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. “Wewe ni kitu gani, ee mlima mkubwa sana? Mbele ya Zerubabeli wewe utakuwa ardhi tambarare. Kisha ataweka jiwe la juu kabisa la mwisho na watu wakipiga kelele wakisema, ‘Mungu libariki! Mungu libariki!’ ”