Zekaria 11:1-3
Zekaria 11:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Fungua milango yako, ewe Lebanoni ili moto uiteketeze mierezi yako! Ombolezeni, enyi misunobari, kwa kuwa mierezi imeteketea. Miti hiyo mitukufu imeharibiwa! Enyi mialoni ya Bashani, ombolezeni, kwa kuwa msitu mnene umekatwa! Sikia maombolezo ya watawala! Fahari yao imeharibiwa! Sikia ngurumo za simba! Pori la mto Yordani limeharibiwa!
Zekaria 11:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ifungue milango yako, Ee Lebanoni, Ili moto uiteketeze mierezi yako. Piga yowe, msonobari, maana mwerezi umeanguka, Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika; Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani, Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia. Sikiza, maombolezo ya wachungaji, Kwa maana utukufu wao umeharibiwa; Sikiza, ngurumo za simba, Kwa maana vichaka vya Yordani vimeharibiwa!
Zekaria 11:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ifungue milango yako, Ee Lebanoni, Ili moto uiteketeze mierezi yako. Piga yowe, msunobari, maana mwerezi umeanguka, Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika; Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani, Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia. Sauti ya wachungaji, ya uchungu mwingi! Kwa maana utukufu wao umeharibika; Sauti ya ngurumo ya wana-simba! Kwa maana kiburi cha Yordani kimeharibika.
Zekaria 11:1-3 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Fungua milango yako, ee Lebanoni, ili moto uteketeze mierezi yako! Piga yowe, ee msunobari, kwa kuwa mwerezi umeanguka; miti ya fahari imeharibiwa! Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani, msitu mnene umefyekwa! Sikiliza yowe la wachungaji; malisho yao manono yameangamizwa! Sikia ngurumo za simba; kichaka kilichostawi sana cha Yordani kimeharibiwa!