Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zek 11

11
1Ifungue milango yako, Ee Lebanoni,
Ili moto uiteketeze mierezi yako.
2Piga yowe, msunobari, maana mwerezi umeanguka,
Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika;
Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani,
Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia.
3Sauti ya wachungaji, ya uchungu mwingi!
Kwa maana utukufu wao umeharibika;
Sauti ya ngurumo ya wana-simba!
Kwa maana kiburi cha Yordani kimeharibika.
Aina mbili za Wachungaji
4BWANA, Mungu wangu, alisema hivi, Lilishe kundi la machinjo, 5#Kum 29:19; Yer 2:3; Hos 12:8; Yn 16:2; 1 Tim 6:9; 2 Pet 2:3ambalo wenye kundi hilo huwachinja, kisha hujiona kuwa hawana hatia; na hao wawauzao husema, Na ahimidiwe BWANA, kwa maana mimi ni tajiri; na wachungaji wao wenyewe hawawahurumii. 6Maana mimi sitawahurumia tena wenyeji wa nchi hii, asema BWANA; bali, tazama, nitawatia, kila mmoja wao, mikononi mwa mwenzake, na mikononi mwa mfalme; nao wataipiga hiyo nchi, wala mimi sitawaokoa mikononi mwao. 7#Sef 3:12; Mt 11:5Basi nikalilisha kundi la machinjo, kweli kondoo waliokuwa wanyonge kabisa.
Kisha nikajipatia fimbo mbili; nami nikaiita ya kwanza, Neema, na ya pili nikaiita, Vifungo; nikalilisha kundi lile. 8#Hos 5:7Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia. 9#Yer 15:2Ndipo nikasema, Sitawalisheni; afaye na afe; atakayekatiliwa mbali na akatiliwe mbali; nao waliosalia, kila mmoja na ale nyama ya mwili wa mwenziwe. 10Nikaitwaa hiyo fimbo yangu, iitwayo Neema, nikaikata vipande viwili, ili nipate kulivunja agano langu nililolifanya na watu wa kabila zote. 11Nayo ikavunjwa siku ile; na hivyo wale kondoo wanyonge walionisikiliza wakajua ya kuwa neno hili ndilo neno la BWANA. 12#Kut 21:32; Mt 26:15Nikawaambia, Mkiona vema, nipeni ujira wangu; kama sivyo, msinipe. Basi wakanipimia vipande thelathini vya fedha, kuwa ndio ujira wangu. 13#Mt 27:9-10Kisha BWANA akaniambia, Mtupie mfinyanzi kima kizuri, hicho nilichotiwa kima na watu hao. Basi nikavitwaa vile vipande thelathini vya fedha, nikamtupia huyo mfinyanzi ndani ya nyumba ya BWANA. 14Ndipo nikaikata vipande viwili fimbo yangu ya pili, iitwayo Vifungo, ili nipate kuuvunja udugu uliokuwa kati ya Yuda na Israeli.
15 # Eze 34:2 BWANA akaniambia, Jitwalie tena vyombo vya mchungaji mpumbavu. 16Kwa maana, tazama, mimi nitainua katika nchi hii mchungaji, ambaye hatawaangalia waliopotea, wala hatawatafuta waliotawanyika, wala hatamganga aliyevunjika, wala hatamlisha aliye mzima; bali atakula nyama ya wanono, na kuzirarua-rarua kwato zao. 17#Yer 23:1; Yn 10:12; Mik 3:6Ole wake mchungaji asiyefaa, aliachaye kundi! Upanga utakuwa juu ya mkono wake, na juu ya jicho lake la kuume; mkono wake utakuwa umekauka kabisa, na jicho lake la kuume litakuwa limepofuka.

Iliyochaguliwa sasa

Zek 11: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha