Zaburi 89:29-33
Zaburi 89:29-33 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wazao wake nao nitawadumisha milele, Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu. Wanawe wakiiacha sheria yangu, Wasiende katika hukumu zangu, Wakizihalifu amri zangu, Wasiyashike maagizo yangu, Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo, Na uovu wao kwa mapigo. Lakini fadhili zangu sitamwondolea yeye, Wala sitafanya uaminifu wangu kuwa uongo.
Zaburi 89:29-33 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nitaudumisha uzao wake milele, kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu. “Kama wanae wataacha amri yangu na wasifuate sheria zangu, kama wakihalifu maagizo yangu na kutoshika amri zangu, nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo, uovu wao kwa kuwapiga, lakini sitauondoa upendo wangu kwake, wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe.
Zaburi 89:29-33 Biblia Habari Njema (BHN)
Nitaudumisha daima ukoo wake wa kifalme, na ufalme wake kama mbingu. “Lakini wazawa wake wakiiacha sheria yangu, wasipoishi kadiri ya maagizo yangu, kama wakizivunja kanuni zangu, na kuacha kutii amri zangu, hapo nitawaadhibu makosa yao; nitawapiga kwa sababu ya uovu wao. Lakini sitaacha kumfadhili Daudi, wala kuwa mwongo kuhusu uaminifu wangu.
Zaburi 89:29-33 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wazao wake nao nitawadumisha milele, Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu. Wanawe wakiiacha sheria yangu, Wasiende katika hukumu zangu, Wakizivunja amri zangu, Wasiyashike maagizo yangu, Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo, Na uovu wao kwa mapigo. Lakini fadhili zangu sitamwondolea yeye, Wala sitafanya uaminifu wangu kuwa uongo.