Zaburi 81:10-12
Zaburi 81:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri. Fumbua kinywa chako, nami nitakulisha. “Lakini watu wangu hawakunisikiliza; Israeli hakunitaka kabisa. Hivyo, nikawaacha wabaki na ukaidi wao; wafuate mashauri yao wenyewe.
Zaburi 81:10-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, Niliyekupandisha toka nchi ya Misri; Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza. Lakini watu wangu hawakuisikiliza sauti yangu, Wala Israeli hawakunitaka. Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao, Waenende katika mashauri yao.
Zaburi 81:10-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, Niliyekupandisha toka nchi ya Misri; Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza. Lakini watu wangu hawakuisikiliza sauti yangu, Wala Israeli hawakunitaka. Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao, Waenende katika mashauri yao.
Zaburi 81:10-12 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mimi ni BWANA Mungu wako, niliyekutoa nchi ya Misri. Panua sana kinywa chako nami nitakijaza. “Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza; Israeli hakutaka kunitii. Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao wafuate mashauri yao wenyewe.