Zaburi 8:3-5
Zaburi 8:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Nikiangalia mbingu, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizozisimika huko, mtu ni nini, ee Mungu, hata umfikirie, binadamu ni nini hata umjali? Umemfanya awe karibu kama Mungu, umemvika fahari na heshima.
Zaburi 8:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha; Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo kuliko Mungu; Umemvika taji la utukufu na heshima
Zaburi 8:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha; Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima
Zaburi 8:3-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota, ulizoziratibisha, mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali? Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni, ukamvika taji ya utukufu na heshima.