Zaburi 7:1-5
Zaburi 7:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA, Mungu wangu, nimekukimbilia Wewe, Uniokoe na wote wanaonifuatia, uniponye. Asije akaipapura nafsi yangu kama simba, Akiivunja-vunja pasipokuwa na wa kuponya. BWANA, Mungu wangu, ikiwa nimetenda haya, Ikiwa mna uovu mikononi mwangu, Ikiwa nimemlipa mabaya Yeye aliyekaa kwangu salama; (Hasha! Nimemponya yeye Aliyekuwa mtesi wangu bila sababu;) Basi adui na anifuatie, Na kuikamata nafsi yangu; Naam, aukanyage uzima wangu, Na kuulaza utukufu wangu mavumbini.
Zaburi 7:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, nakimbilia usalama kwako; uniokoe na wote wanaonidhulumu, unisalimishe. La sivyo, watakuja kunirarua kama simba, wakanivutia mbali, pasiwe na wa kuniokoa. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu! Kama nimetenda moja ya mambo haya: Kama nimechafua mikono yangu kwa ubaya, kama nimemlipa rafiki yangu mabaya badala ya mema, au nimemshambulia adui yangu bila sababu, basi, adui na anifuatie na kunikamata; ayakanyage maisha yangu; na kuniulia mbali.
Zaburi 7:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA, Mungu wangu, nimekukimbilia Wewe, Uniokoe na wote wanaonifuatia, uniponye. Asije akaipapura nafsi yangu kama simba, Akaniburura hadi pasipokuwa na wa kuniponya. BWANA, Mungu wangu, ikiwa nimetenda haya, Ikiwa mna uovu mikononi mwangu, Ikiwa nimemlipa mabaya Yeye aliyekaa kwangu salama; (Hasha! Nimemponya yeye Aliyekuwa mtesi wangu bila sababu;) Basi adui na anifuatie, Na kuikamata nafsi yangu; Naam, aukanyage uzima wangu, Na kuulaza utukufu wangu mavumbini.
Zaburi 7:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA, Mungu wangu, nimekukimbilia Wewe, Uniokoe na wote wanaonifuatia, uniponye. Asije akaipapura nafsi yangu kama simba, Akiivunja-vunja pasipokuwa na wa kuponya. BWANA, Mungu wangu, ikiwa nimetenda haya, Ikiwa mna uovu mikononi mwangu, Ikiwa nimemlipa mabaya Yeye aliyekaa kwangu salama; (Hasha! Nimemponya yeye Aliyekuwa mtesi wangu bila sababu;) Basi adui na anifuatie, Na kuikamata nafsi yangu; Naam, aukanyage uzima wangu, Na kuulaza utukufu wangu mavumbini.
Zaburi 7:1-5 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, ninakukimbilia wewe, uniokoe na kunikomboa na wote wanaonifuatia, la sivyo watanirarua kama simba na kunichana vipande vipande, asiwepo wa kuniokoa. Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, kama nimetenda haya na kuna hatia mikononi mwangu, au ikiwa nimemtenda uovu aliye na amani nami, au nimemnyang’anya adui yangu pasipo sababu, basi adui anifuatie na kunipata, auponde uhai wangu ardhini na kunilaza mavumbini.