Zaburi 69:6-9
Zaburi 69:6-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe, Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi. Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe, Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli. Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu. Maana wivu wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.
Zaburi 69:6-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Wanaokutumainia wasiaibishwe kwa sababu yangu, ee Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi; wanaokutafuta, wasione fedheha kwa sababu yangu ee Mungu wa Israeli. Kwa ajili yako nimefedheheshwa, aibu imefunika uso wangu. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, kaka na dada zangu hawanitambui. Upendo wangu kwa nyumba yako unanimaliza. Kashfa zote wanazokutolea wewe zimenipata mimi.
Zaburi 69:6-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe, Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi. Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe, Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli. Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na asiyetambuliwa na wana wa mama yangu. Maana mvuto wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.
Zaburi 69:6-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee Bwana, ewe BWANA Mwenye Nguvu Zote, wakutumainio wasiaibishwe kwa ajili yangu; wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli. Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako, aibu imefunika uso wangu. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe. Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila, matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia.